HADITHI
YAMENIKUTA SALMA MIE 14
ILIPOISHIA
Nilipotoka nje nilimkuta yule
kijana akinisubiri kwenye gari. Aliponiona alinifungulia mlango wa upande wa
pili wa dereva akaniambia.
“Ingia twende”
Nikaingia kwenye gari na
kufunga mlango.
Kijana huyo akaliwasha gari tukaondoka.
Kupata hiyo lifti nilishukuru sana
kwani ningeweza hata kurudi nyumbani kwangu kwa miguu.
“Mimi naitwa Chinga, sijui
mwenzangu unaitwa nani?” Kijana huyo akaanza kuniuliza.
“Miye naitwa Salama”
nikamjibu.
“Huyo mwenye matatizo ni mume
wako?” akaniuliza.
“Ndiyo ni mume wangu”
“Ana matatizo gani?”
“Amepofuka macho. Na sababu
ya kupofuka ni dawa nilizopewa na mzee. Dawa ambayo niliambiwa nimtilie kwenye
chakula nilimtilia kwenye maji ya kuoga.
Baada ya kuoga yale maji, macho yalipofuka hapo hapo”
Kijana huyo nilipomwambia
hivyo alitikisa kichwa kusikitika.
“Ulipomueleza mzee
alikwambiaje?”
SASA ENDELEA
Alinipa dawa nimfanyie lakini
hazikusaidia. Hivi sasa maisha
yamekuwa magumu kwa sababu
mume wangu hawezi kufanya
kazi. Tumehangaika
mahospitalini bila mafanikio. Pesa zote
zimetuishia. Hivi
tunavyozungumza umeme pia umekatwa
nyumbani kwa sababu tumeshindwa kulipia bili”
Chinga alikuwa akinisikiliza huku akitikisa
kichwa kusikitika
“Sasa leo umepewa dawa gani?”
“Leo ameniambia kuwa mume wangu amerogwa na
wenzake,
ndio amenipa hii mzizi
nikamchemshie kwa siku saba. Sasa hilo
si
tatizo, tatizo ni kuwa baada
ya hizo siku saba mganga ametaka
niende na shilingi laki
mbili. Nitazitoa wapi?”
“Kweli ni tatizo” Chinga akanikubalia.
“Kama
nitashindwa basi, nitashukuru tu”
Chinga alinyamza kimya. Bila shaka alikuwa
akinionea huruma.
“Unaishi maeneo gani?” akaniuliza baada ya
ukimya mfupi.
“Tunaishi Usagara”
"Ngoja nikupeleke"
"Usinifikishe nyumbani kabisa.
Nitakuonesha mahali pa
kunishusha"
nikamwaambia. Akanielewa.
Wakati tunaelekea Usagara aliniambia.
"Mimi ninaishi Dar, nimekuja mara moja
tu kumsalimia baba. Pengine keshokutwa nitaondoka"
"Kumbe yule ni baba yako mzazi?"
nikamuuliza.
"Ni baba yangu mzazi isipokuwa mama
yangu alikufa"
"Kwa hiyo yule aliyenaye pale ni mama
yako wa kambo?"
"Yule
ni mama wa kambo"
"Vizuri sana"
Pakapita kimya kifupi kabla ya Chinga
kuniuliza tena
"Utarudi lini tena kuchukua
dawa?"
"Nimeambiwa nirudi baada ya siku saba"
"Huenda nikawa nimeshaondoka"
akaniambia na mimi sikumjibu kitu.
Tulipofika Usagara nilimwambia
anishushe kwenye kituo cha daladala. Tukaagana hapo hapo. Akaenda zake na mimi
nikaenda nyumbani kwangu.
Nilipofika nyumbani nilimdanganya mume wangu
kuwa dawa hizo nilipewa na bibi yangu ambaye alikuwa ni mtabibu. Akaamini.
Kama
nilivyoagizwa na mganga nilimchemshia mume wangu dawa hizo kwa siku saba.
lakini kama zilivyokuwa dawa za mwanzo hazikuleta
mafanikio yoyote. Niliona uvivu kurudi tena kwa yule mganga, nikawa sijui la
kufanya.
Siku zikapita. Maisha ya nyumbani yakawa ya
tabu zaidi na ya kukata tamaa. Siku moja walikuja maofisa wa benki nyumbani
kumtafuta mume wangu. Kumbe Ibrahim alikuwa akidaiwa mkopo wa benki ambao
ulikuwa umepita nuda wake wa kulipa. Ile nyumba yetu ndiyo alikuwa ameiwekea
dhamana ya mkopo. Masafisa hao wakamwaambia kwamba walikuwa wanahitaji pesa zao.
Mume wangu akaomba kusubirishiwa kidogo
kutokana na hali yale lakini maofisa hao wa benki walikataa kumuongezea muda
kwa madai kuwa riba itazidi kuongezeka na kutokana na hali yake hatoweza kulipa.
Walimpa wiki moja za kulipa pesa alizokuwa anadaiwa, vinginevyo walimwaambia
nyumba yetu ingenadiwa kufidia deni hilo.
"Macho yangu yangekuwa mazima
yasingenikuta hayo, ningeweza kulipa deni hilo
na hata kama ningeomba muda zaidi wangenikubalia"
mume wangu akaniambia kwa masikitiko.
"Sasa tufanyeje mume wangu, nyumba hii
ikinadiwa tutaenda kuishi wapi?" nikamuuliza.
Mume wangu hakuwa na la kujibu. Kumbe
Ibrahim alikuwa akimiliki kiwanja pale pale Usagara lakini kilikuwa ni siri yake.
Ikabidi anieleze. Ili kuokoa nyumba yetu isiuzwe
ilimbidi auze kiwanja hicho. Pesa
iliyopatikana akalipia deni alilokuwa anadaiwa. Nyumba yetu ikasalimika.
Kutokana na maisha kuendelea kuwa ya dhiki
nikarudi tena kwa yule mganga. Nikamueleza matatizo yaliyokuwa yanatukabili
kutokana na mume wangu kutoona.
"Kama
angekuwa anaona angeendelea na kazi zake na pesa ingepatikana lakini sasa
hawezi kufanya kazi" nilimwaambia. mganga huyo kwa kusikitika.
Mganga huyo hakuchoka kunipa dawa. Kama kawaida yake akanipa dawa nyingine ya utomvu utomvu,
akaniambia nichanganye na rangi ya chai kisha nimpake kwenye macho yake asubuhi
na jioni kwa siku tatu.
Nikarudi nyumbani. Nikamfanyia mume wangu
dawa hiyo kwa siku tatu kama nilivyoagizwa na
mganga huyo, lakini pia haikuleta mafanikio yoyote.
Nikataka kurudi nikamueleze mganga huyo
lakini nikawa sina nauli.
Siku moja nilikuwa nimekwenda sokoni. Wakati
ninarudi nyumbani nikaona gari inanifungia breki miguuni, nikashituka. Nilipotupa
macho nikaona ni ile Rav 4 ya yule kijana niliyekutana naye siku ile kwa yule
mganga.
Akatoa kichwa kwenye dirisha la gari na
kunisalimia.
“Asalaam alaykum”
"Alaykum salaam" nikamjibu huku
nikitabasamu.
"Habari za huko?" nikamuuliza
"Nzuri. Ingia nikusindikize"
akaniambia.
Nikazunguuka upande wa pili wa gari
nikajipakia.
"Umekuja lini?" nikamuuliza.
"Nimekuja juzi"
"Mzee hajambo?"
"Hajambo"
"Nilikuwa nataka kwenda kumuona
nimjulishe hali ya mgomjwa lakini sijapata nafasi" Nilisingizia nafasi lakini
ukweli ni kuwa sikuwa na pesa ya nauli.
"Kwani yule bwana mpaka sasa
hajapona?"
"Bado hajapona. Tuna hali mbaya kweli
hivi sasa!"
"Ninakuona, sivyo ulivyokuwa"
ITAENDELEA kesho usikose kujua utomvu utomvu Salma alopmpaka mume wake nini kitatokea
No comments:
Post a Comment