Programu mpya ya Facebook kuzinduliwa Kenya
Facebook imezindua aina mpya ya programu tumishi yake ya kutuma ujumbe ambayo inawalenga watu wa mataifa yanayoendelea.
Programu
hiyo mpya ya Messenger, ambayo inaitwa Messenger Lite, itaanza kutumiwa
nchini Kenya, Tunisia, Malaysia, Sri Lanka na Venezuela kwanza.Itazinduliwa katika nchi nyingine baadaye.
Messenger Lite imeundwa kutotumia sana data, jambo ambalo huwa tatizo kubwa mataifa yanayoendelea kutokana na gharama pamoja na kasi ya mtandao.
Programu hiyo ya simu za Android pia inaweza kufanya kazi kwa urahisi maeneo ambayo huduma ya mtandao si ya kutegemewa.
"Messenger Lite ukubwa wake ni chini ya 10MB, hivyo ni rahisi sana kuiweka kwenye simu na kuifungulia," taarifa ya Facebook imesema.
No comments:
Post a Comment