Thursday, January 15, 2015

FLOYD MAYWEATHER V/S MANNY PACQUAIO?

Floyd Mayweather vs Manny Pacquaio?

Frontpage072110 copy copy.eps

Pambano la Masumbwi linalosubiriwa na ulimwengu mzima kati ya mabondia wawili bora katika miaka ya hivi karibuni linakaribia kutokea baada ya uthibitisho wa mazungumzo ya pande mbili zinazowakilisha mabondia hao .
Wakala wa Bondia Mfilipino Manny Pacquiao Fred Sternburg amethibitisha kuwa mazungumzo baina ya kambi za mabondia hawa wawili yanaendelea vizuri na huenda makubaliano yakafikiwa siku sio nyingi .
Manny Pacquaio amewahi kutwaa mataji kwenye madaraja nane tofauti ya uzito .
Manny Pacquaio amewahi kutwaa mataji kwenye madaraja nane tofauti ya uzito .
Wakala huyo hata hivyo amekanusha kuwepo kwa uthibitisho wa tarehe ya mabondia hao kupanda ulingoni baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa wawili hao watapambana Mei mbili mwaka huu .
Pambano hili limewahi kuandaliwa kwa muda mrefu bila mafanikio baada ya mabondia hawa kuonekana wakikwepana hususan Floyd ambaye alikuwa akitoa visingizio vya kila aina ikiwemo kutaka mpinzani wake apimwe vipimo vya dawa za kulevya .
Floyd Mayweather ameingia ulingoni mara 47 na hajawahi kupoteza pambano hata moja .
Floyd Mayweather ameingia ulingoni mara 47 na hajawahi kupoteza pambano hata moja .
Taarifa zaidi zinasema kuwa mabondia hawa wamekubaliana kugawana asilimia 60 kwa 40 ya mapato ya pambano hili ambapo Floyd atachukua asilimia 60 na Manny atachukua asilimia 40 .
Yote haya unayapata kupitia,tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment