Nimekuwekea Hekaheka ya leo Jan 15, inahusu mtoto anayeteswa na Mama yake
Kama
hukusikiliza Hekaheka ya leo Jan 15 inatokea Kunduchi, Dar inahusu mama
ambaye inasemekana amekuwa akimtesa mtoto wake kwa kumpiga kitendo
kilichowachosha majirani na kuamua kumchukua mtoto huyo.
Mtoto huyo amesema kuwa mama yake
amekuwa akimpiga kwa banio la kupigia ugali, chupa na waya ambapo mara
ya mwisho alimpiga kwa kumtuhumu kumuibia fedha baada ya kumtuma
dukani.
Mama huyo alipoulizwa amesema mtoto huyo
alikuwa na tabia za ajabu toka akiwa mdogo na amekuwa akimpiga kwa
fimbo ili ajirekebishe japo majirani hawakukubaliana na utetezi wa
mwanamke huyo.
Baba ambaye ni jirani aliyemchukua
mtoto huyo amesema tayari amepeleka suala hilo Polisi na amepeleka barua
kwa mjumbe ili aweze kukaa na mtoto huyo kwa kufuata utaratibu
unaotambulika.
No comments:
Post a Comment