Pale ambapo Chifu anahusishwa na wizi huu Kenya…
“Ameshikwa kwa sababu alibomoa stoo ya chakula na kuchukua chakula kashikwa akiwa na mafuta ya three little ya kupikia chakula”– Mwananchi.
Licha ya Chifu huyo kuwa na funguo ya
ghala hilo aliamua kuvunja mlango wa ghala hilo kwa lengo la kuficha
ushahidi, lakini Polisi waliokuwa doria wakamkuta akiwa amebeba vitu
mbalimbali na kumkamata.
Wakazi wa eneo hilo wamesema tabia ya
wizi wa chakula cha msaada umekithiri sana huku wakilalamika kuwa hata
kidogo kinachopatikana watu hupeana kwa kujuana huku walioathirika kwa
njaa wakikosa, wengine hula mizizi,
Chifu huyo alipelekwa kituo cha Polisi kwa ajili ya kupelekwa Mahakamani.
No comments:
Post a Comment