Stori kubwa muhimu zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania January 16, 2015
MWANANCHI
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC imeitaka Menejimenti ya Mamlaka ya bandari TPA
kurejesha nyongeza ya fedha zote za malipo za safari zilizowalipa
watendaji wake tangu mwaka 2011 baada ya kubaini kuwa zililipwa bila
kuidhinishwa na msajili wa Hazina.
Ukaguzi maalum uliofanywa katika mamlaka
hiyo na Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali CAG mwaka
2011/12, unaonyesha kuwa TPA iliomba nyongeza ya malipo
ya safari lakini kabla ya kupewa kibali na msajili wa Hazina, ilianza
kuwalipa watendaji wake nyongeza hiyo.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe
alisema malipo ya safari kwa wafanyakazi wa ngazi za chini wa Mamlaka
hiyo kwa siku awali walikua wakilipwa 94,000 na sasa ni 123,000 na
watendaji wa juu awali walikua wakilipwa 270,000 na sasa ni 500,000.
Alisema malipo kwa safari za nje watendaji wa ngazi za chini kwa siku
ni dola za Marekani 296 na wale wa ngazi za juu ni dola 600 awali na
sasa dola 800.“Tunataka mrejeshe fedha hizi tangu mlipoanza kuzilipa mwaka 2011 kwa sababu mlifanya makosa kwani mmelipa bila kupewa kibali na msajili wa hazina” alisema Zitto.
MWANANCHI
Jumuiya wa wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es salaam UDASA na ITV, Radio One wamesaini makubaliano ya kuandaa mdahalo wa wagombea wa Urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Mwenyekiti wa UDASA, Prof. Kitila Mkumbo alisema katika nchi za kidemokrasia midahalo hufanikisha uchaguzi ulio huru, haki na uwazi.
Pia alisema midahalo hiyo hutoa fursa
muhimu kwa wagombea kueleza falsafa, sera na mikakati yao ya kutatua
matatizo mbalimbali yanayowakalibi wananchi.
Aidha alisema midahalo watakayoendesha haitaegemea upande wowote na kwamba mgombea atakayekataa kushiriki hawatamlazimisha.
MWANANCHI
Wanafunzi watatu wa mwaka wa tatu ambao ni viongozi wa Chuo kikuu cha Dodoma UDOM wametimuliwa kwa madai ya kuwa chanzo cha migogoro chuoni hapo.
Makamu Mkuu wa UDOM, Prof. Idris Kikula alisema jana waliwafukuza wanafunzi hao kwa kosa la kuwa kinara wa kushinikiza migomo.
Kwa upande mwingine wanafunzi 84 wa
programu maalum ya Stashahada ya ualimu chuoni hapo waliofanya mgomo na
kushinikiza kulipwa madai yao, jana walipandishwa kizimbani katika
mahakama ya Mkoa wa Dodoma kwa kosa la kukusanyika bila kibali.
Hakimu mkazi Kabate Richard alisema
dhamana ipo wazi kwa wanafunzi hao ambao walijidhamini wenyewe kwa
shilingi 20,000 na sasa kesi hiyo itasikilizwa tena February 16-19 mwaka
huu.
MWANANCHI
Jeshi la Polisi Kibaha limewakamata raia 14 wa Ethiopia kwa tuhuma za kukutwa katika moja ya vichaka lililopo eneo la TAMCO wakiwa hawana vibali vya kuingia nchini.
Kamada wa Polisi Pwani Ulrich Matei alisema
wahamiaji hao waliingia nchini wakitokea Kenya na walisafiri kwa
kutumia gari aina ya fuso hadi Wilaya ya Bagamoyo walipotelekezwa kwenye
moja ya mapori katika barabara ya TAMCO.
Alisema Polisi kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji waliwabaini wahamiaji hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Katika maelezo yao raia hao walisema
wamekimbia njaa na vita nchini mwao na walikua wakijiandaa kusafiri
kimya kimya hadi Afrika Kusini kutafuta kazi.
MTANZANIA
Kamati ya Nishati na Madini imeonyesha
hofu juu ya Jiji la Dar es salaam kuteketea kwa moto kutokana na
uwezekano wa kulipuka kwa mabomba ya kusafirishia mafuta unaohusisha
utoboaji wa mabomba hayo.
Kutoka na hali hiyo Wabunge wameomba vyombo vya ulinzi hususani JKT na JWTZ
kupewa jukumu la kuimarisha miundombinu ya kusafirisha mafuta huku
baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakijiandaaa kuhamisha familia zao Dar.
Hofu ya Wabunge hao ilitokana na taarifa iliyosomwa mbele yao na meneja mkuu wa Makampuni yanayoingiza mafuta nchini, Michael Minja kwa ajili ya kutolea ufafanuzi punguzo la bei ya mafuta katika soko la dunia.
Katika sehemu ya taarifa hiyo Minja alisema mafuta yanapotea njiani baada ya kuibiwa yanakuwa yameshalipiwa kodi hali inayofanya waagizaji wabebe hasara hiyo.
“Mbali na kuibwa,hatuombi litokee lakini kwa namna miundombinu ya kusafirisha mafuta ilivyo,jiji lote litaangamia“alisema Minja.MTANZANIA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magessa Mulongo anaishi katika hoteli ya utalii yenye hadhi ya nyota nne kwa miezi miwili sasa kutokana na nyumba yake kuhitaji ukarabati.
Tangu alipowasili Mwanza mara baada ya mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete,
Mkuu huyo wa Mkoa amekua akiishi katika hotel ya kitalii ya Malaika
yenye hadhi ya nyota nne ambayo chumba kimoja kwa siku hutozwa sh
425,000 au milioni 25.5 kwa mwezi.
Mulungo alisema nyumba aliyokua akiishi
inahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa kutokana na kutofanyiwa kwa muda
mrefu kwa sababu ya uhaba wa fedha hivyo kuwa katika hali mbaya.
“Nimesikua mengi yanasemwa kuhusu
jambo hili lakini sitaki kuingia katika malumbano yasiyo na tija,unaweza
kuwasiliana na watu wa TBA ambao ni wakala wa majengo“alisema Mulongo.HABARILEO
Mamlakaya Udhibiti wa Nishati ya maji, EWURA
imebainisha kuwa hadi kufikia March mwaka huu bei ya mafuta nchini
itaendelea kushuka kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta kwenye soko la
dunia.
Hata hivyo Mamlaka hiyo imeonya bei hiyo
ya mafuta haitaweza kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kushuka kwa
thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani pamoja na kutobadilika kwa
ushuru mbalimbali wa ndani wa mafuta.
Akiwasilisha taarifa ya ukokotaji wa mafuta kwa kamati, Mtaalamu kutoka EWURA, Lorivii Long’idu alikiri ni kweli kwa sasa bei ya mafuta katika soko la dunia imekua ikishuka kwa kasi ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
“Bei
hizi zimeshuka kutoka sola 100 hadi kufikia dola 60 kwa pipa ambayo ni
sawa na asilimia 40 kutokana na kudorora kwa uchumi wa bara la Ulaya
katika kipindi hiki na kuwepo kwa tofauti za mitazamo ya kisiasa hasa
katika nchi za Marekani na Urusi,”alisema Long’idu.
NIPASHE
Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa imeandikia barua Chama cha Tanzania Labour Party TLP, kukitaka kifanye uchaguzi wa viongozi na kwamba endapohakitafanya hivyo kitafutiwa usajili.
Msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza
alisema sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 kifungu cha 9 inavitaka
vyama hivyo kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano lakini chama
hicho kimepitisha muda bila kufanya uchaguzi.
Alisema ofisi ya msajili ilipokea maombi
kwa chama hicho mara tatu kikiomba kusogezewa mbele muda wa kufanya
uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali.
Sababu ya kwanza ilikuwa Mwenyekiti wake, Augustine Mrema
kuwa nje ya nchi kwa matibabu, sababu ya pili ilikuwa kupisha Bunge
maalum la Katiba na nyingine ilikua uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment