Steven Gerard atacheza wapi baada ya kuagana na Liverpool?
Zikiwa zimepita saa 24 tangu nahodha wa zamani wa England Steven atangaze kuwa ataachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu imefahamika kuwa kiungo huyo atasajiliwa na klabu ya nchini Marekani.
Taarifa hii inakuja kama uthibitisho wa tetesi ambazo zilisikika tangu awali kwamba Gerrard angesajiliwa na timu inayoshiriki ligi ya Marekani maarufu kama MLS kama ambavyo imekuwa kawaida kwa nyota kadhaa ambao hukaribia kumaliza nyakati zao za kucheza soka la ushindani barani ulaya .
Timu ambayo imetajwa sana kuwa na nia ya kumsajili Gerard ni Los Angeles Galaxy moja ya klabu maarufu kuliko zote kwenye ligi ya Marekani .
Umaarufu wa Galaxy uliongezeka maarufu wakati klabu hiyo ilipomsajili nyota wa zamani wa Manchester United David Beckham wakati alipomaliza mkataba wake na klabu ya Real Madrid.
Hakuna ubishi kuwa Becks aliiongezea umaarufu ligi ya marekani hali ambayo imechangia kuwavuta nyota wengine kusajiliwa na timu kadhaa za ligi hiyo .
Steven
Gerard siku ya ijumaa alitangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa
msimu huu baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.
No comments:
Post a Comment