Huduma ya dharura kwa watumishi wa umma Kenya imeboreshwa, kwa sasa zinatumika na ndege mtu wangu!
Vifaa
vya uokoaji ni vitu muhimu katika jamii hasa pale matatizo yanapotokea,
ni vizuri msaada ukapatikana mapema pale ambapo unahitajika, Serikali
ya Kenya imeamua kufanya hili kama moja ya njia za kuboresha huduma ya
dharura kwa watumishi wa huduma za kiafya.
Tumesikia malalamiko mengi kutoka kwa
watumishi wa Serikali kuhusu huduma mbaya wanazopatiwa mbali na kuwa
wanakatwa kodi kubwa kila mwezi.
Kenya wamezindua huduma za dharura kwa
kutumia Ndege na magari ya kisasa kwa watumishi wa umma, uzinduzi wa
huduma hiyo uliohudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Huduma hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano
na Shirika la Bima ya Afya, Shirika la Msalaba Mwekundu na kundi la
madaktari wanaosafiri kwa ndege la AMREF.
Huduma hiyo inafanya Kenya kuwa nchi ya pili baada ya Afrika Kusini kutoa huduma ya aina hii.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment