Baada ya meneja kuongea, Wema Sepetu mwenyewe kaongea kuhusu ishu ya kumpeleka Diamond Polisi.
Kwenye Exclusive Interview na millardayo.com Wema Sepetu ameyasema haya >>>“Hii taarifa
imenishtua sana maana asubuhi ya jana nimekuta kwenye gazeti wameandika
nikashangaa yaani hapa nimekaa kwa sababu muda mwingi siendeshi mimi
akaunti yangu ya twitter, anaiendesha mtu wangu wa blog Bestizo maana
nilikua nataka kutoa tamko“
“Nilishasema
ukurasa huu tulishaufunga na nilishasema haiwezi kujirudia tena,
nashangaa watu wanarudi na maneno yale yale maana nimekaa kimya kwa kila
kitu ili kuepuka haya maneno“
“Sijawahi
kujiunga VICOBA maana sivijui, nilikua nimekaa na mtu akanambia labda
Wema hujui hawa watu wa VICOBA wanajaribu kujitangaza kwa njia hii na
kutengeneza hii kitu kwamba VICOBA wanaweza kukopa hadi Milioni kumi…
kwanza mimi siwezi kukopa Milioni 10..“– Wema Sepetu.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment