Muigizaji wa Bongo Movie Aunty Ezekiel
Soudy Brown amepiga story na muigizaji Aunty Ezekiel kuhusiana
taarifa kwamba ni mjamzito na ameonekana akinywa pombe, Soudy
alimuuliza kama anafahamu athari za kunywa pombe huku akiwa na ujauzito,
Aunty akasema hazijui na yeye sio mjamzito.
Soudy alimtafuta pia Dk Makongoro kutoka
Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye alielezea kuhusu matatizo ambayo
mwanamke anaweza kuyapata iwapo ni mjamzito na anatumia pombe kali,
daktari huyo amesema kuwa mama mjamzito anatengeneza mazingiza ya pombe
kusafiri kutoka kwake kwenda kwa mtoto na kujitunza kwenye sehemu za
ubongo kitendo kinachosababisha mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo kama
mtindio wa Ubongo, Kuzubaa au matatizo ya macho.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari wakati wowote kukupatia kinachijiri kila pembe ya nchini na ulimwenguni kote kupitia tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment