Kauli ya Waziri Chikawe kuhusiana na Waganga wanaochangia mauaji ya Albino
Waziri wa mambo ya ndani Mathias Chikawe ametoa tamko kuwa kutakua na operesheni ya kitaifa ya kuwasaka na kuwakamata waganga wa kienyeji maarufu kama wapiga ramli ili kuwafikisha mahakamani.
Uamuzi wa Waziri huyo unatokana na kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa watu wenye ulemavu vikishika kasi kutokana na kuuawa kwa imani za kishirikina.
Chikawe alisema watashirikiana na Chama cha watu wenye ulemavu TAS kuwabaini wahalifu na kuwachukulia hatua ili kupunguza vitendo hivyo.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment