Thursday, January 15, 2015

BOB JUNIOR , NEY WAMITEGO WATOA KALI

Wasanii Bob Junior, Ney Wamitego,Witness ni kati ya waliosikika kwenye 255 ya leo jan 15.

El Perfect
Ile collabo kati ya msanii Bob Junior  na Jose Chameleone tayari imeshapikwa katika studio mbili, Sharobaro Record na Island Record ambapo Bob Junior amefunguka kwenye 255 kuwa ni ngoma kubwa  ingawa imechelewa kutoka kutokana na burdget ya video kuwa kubwa, wimbo utakuwa tofauti na wa Kiafrika zaidi.
Bob Junior amekanusha tetesi za kutoka na mwigizaji Wema Sepetu  na kusema ni mtu ambaye wanashirikiana kwenye mambo mengi.
Msanii Ney Wamitego amezungumza kuhusu msanii wa Afrika Kusini,  Zola kukataa kufanya remix ya ‘Akadumba’ na badala yake alimshauri wafanye wimbo mpya ambao tayari wamesharekodi.
Witness na mpenzi wake Ochu Sheggy  ambao wameachia wimbo wao mpya, wamepiga story na 255  kutokana na kuonekana kuongozana muda wote na kuwauliza mastaa gani wanaowa-inspire jinsi wanavyoishi, wawili hao walisema wanavutiwa na  Brad Pitt na Angelina Jollie kutokana na kwamba wanafanya kazi kwa pamoja ingawa ni wapenzi lakini wanaheshimiana, upande wa mastaa wa muziki wanavutiwa na Jay Z na Beyonce.
Jarida la International Business Times 2013 liliripoti kuwa   utajiri wa Jay Z na Beyonce unakadiriwa kufika dola bilioni moja na kuwafanya kuwa Pop First Billionaire Couple.

No comments:

Post a Comment