Rais wa Equatorial Guinea ameamua kutoa zawadi hii kwa mashabiki kuelekea AFCON
Rais wa nchi hiyo Teodoro Obiang Nguema ameamua kununua tiketi 40,000 ambazo zina gharama ya milioni 20 kwa ajili ya kuwapa mashabiki ambao hawatakua na uwezo wa kulipia tiketi ili kuweza kuona mashindano hayo.
“Lazima tuonyeshe kujali mashindano makubwa kama haya, tunahitaji kwenda kwa wingi uwanjani ili kujaza uwanja na kutoa hamasa “alisema mkuu huyo wa nchi.
Alisema ili kuongeza hamasa zaidi Serikali yake itatoa muda kwa wafanya kazi kutoka mapema ili kuweza kuhudhuria mechi zitakazokua zikichezwa siku za kazi.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment