Enjoy na story za kwenye 255 ya leo Jan 20, ziko story za Jay Moe, January Makamba
Kwenye 255 ya leo January 20 wa kwanza kusikika ni Naibu Waziri Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba,
amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais atapambana na matukio ya rushwa
kwa kuanza kuutafuta ukweli na kisha kutoa adhabu kwa wahusika na kwa
kuwa sekta hiyo ina mapungufu kuna haja ya kuurekebisha mfumo mzima
unaopambana na vitendo vya rushwa.
Rapper Songa amefunguka
juu ya kukwama kwa project aliyoianzisha mwaka jana ya kutambulisha
wimbo mpya kila wiki na kusema kilichokwamisha ni kutokana na masuala ya
kifamilia yaliyomfanya asafiri na kuwa kijijini ambapo hamna studio
kitendo kilichokwamisha project hiyo.
Rapper mkali na mkongwe Tz, Jay Moe amesema alishindwa kutoa album yake ya Mocumentary
kama alivyokuwa ameahidi zaidi ya miaka mitatu iliyopita kutokana
kukosekana mwamko kwa wasanii kutoa album badala yake wamekuwa wakirelease
sana nyimbo kutokana na kubadilika kwa biashara ya muziki Tz, kwa sasa
atakuwa akiachia nyimbo mbili mbili kutoka kwenye album hiyo mpaka
ziishe.
No comments:
Post a Comment