Sasa kuna hii inayosema mitandao ya kijamii ni kipimo cha stress na pressure…
Moja
ya Teknolojia inayokua kwa kasi ni matumizi ya mitandao ya kijamii
duniani kote ambapo kwa sasa mamilioni ya watu wamekua wakitumia
mitandao hiyo kuwasiliana.
Lakini unaambiwa watafiti kutoka Australia wamegundua kuwa matumizi ya mitandao husaidia kumtambua mgonjwa wa moyo pamoja na mtu mwenye stress kwa asilimia kuwa.
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Melbourne na Pennsyvania, Marekani unaonyesha kuwa post za kwenye kurasa za mitandao kama Twitter sio tu zinaweza kuonyesha hatari ya ugonjwa wa moyo lakini pia zinaweza kutumika kama kipimo cha saikolojia.
Matokeo
ya utafiti huo ambayo yatachapishwa wiki ijayo katika jarida la
kisayansi yameonyesha kuwa kutumia maneno mazuri katika mitandao
kunaweza kubainisha mambo mengine yanayohusu afya ya mtu.
Mfano kwenye ukurasa wa Facebook sehemu ya kuandika post, kuna option imeandikwa ‘Add what you’re doing or feeling‘, ukiandika ‘annoyed’, ‘sad’ au ‘emotional‘ moja kwa moja inahusisha na hatari ya kupata magonjwa ya moyo, lakini maneno ‘blessed’, ‘loved’ au ‘happy‘ yanakuweka kwenye hatari ndogo ya magonjwa hayo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment