Friday, January 23, 2015

TAARIFA KUTOKA SAUDI ARABIA

Majonzi kwa watu wetu Saudi Arabia, wamepata msiba wa kiongozi wao

486887_1280x720
Siku ya jana January 22 tumeshuhudia Zambia wakifanya uchaguzi wa Rais baada ya Rais wao Michael Chilufya Sata kufariki akiwa madarakani mwaka 2014, hiyo ilikuwa mara ya pili Zambia kupata msiba wa Rais wao akiwa madarakani, wa kwanza alikuwa Levy Mwanawasa aliyefariki mwaka 2008.
Taarifa sio nzuri kutoka Saudi Arabia, vyombo vikubwa vya habari kama CNN, Sky News na BBC vinaripoti kuhusu msiba wa aliyekuwa Mfalme wa  Saudi Arabia, Abdullah Bin Abdulaziz ambaye amefariki akiwa Hospitalini akipatiwa matibabu, taarifa za kifo cha mfalme huyo zimetolewa na kaka yake Salman ambaye naye aliwahi kuwa mfalme.
Kabla ya taarifa za kifo hicho Television ya Taifa la Saudia ilikatisha matangazo yake na kuweka nyimbo za maombolezo kama ishara ya kifo cha kiongozi wa juu, King Abdullah alilazwa hospitali tangu December mwaka  jana kutokana ugonjwa wa mapafu, amefariki  akiwa na umri wa miaka 90.
Mfalme huyo aliingia madarakani mwaka 2005, ni mfalme wa  tano kutoka kwenye familia yake.
Viongozi mbalimbali Duniani wametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo hicho akiwemo Rais wa Marekani Barack Obama na Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron.
Serikali ya Saudi Arabia imetangaza kuwa mazishi ya Mfalme huyo yatafanyika leo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment