Majeruhi ya wachezaji hawa yanawaweka kwenye wakati mgumu Arsenal kwa sasa…
Klabu ya Arsenal
imekumbwa na janga lingine la majeruhi baada ya ripoti kuhusu wachezaji
wake wawili muhimu kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu wakiuguza
majeraha tofauti.
Arsenal itawakosa kiungo mkongwe ambaye pia ni nahodha wa timu, Mikael Arteta
ambaye amefanyiwa upasuaji wa kuondoa mfupa mdogo kwenye kifundo chake
cha mguu na atahitaji miezi mitatu ya kupumzika kabla ya kurudi
uwanjani.
Ukiachilia mbali Arteta, the Gunners pia watamkosa beki wa kushoto Matthieu Debuchy ambaye amefanyiwa upasuaji wa kurekebisha bega lake baada ya kuteguka kwenye mchezo dhidi ya Stoke City uliopigwa jumapili ya wiki iliyopita.
Beki wa kushoto wa Arsenal Mfaransa Mathieu Debuch naye atakaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kuumia bega .
Hii ni mara ya pili kwa Debuchy kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya nyota huyo wa Ufaransa ambaye yuko kwenye msimu wake wa kwanza ndani ya Arsenal kuumia kifundo cha mguu hapo awali ambapo alikaa nje ya uwanja kwa kipindi kama hiki.
No comments:
Post a Comment