Thursday, January 15, 2015

SOMA HABARI KUU ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO, TZ

Mkusanyiko wa Stori muhimu zilizoandikwa na Magazeti ya leo Tanzania January 15, nimekuwekea hapa

locNIPASHE
Jeshi la Polisi jana lilifyatua mabomu kuwatawanya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (Udom) waliokua wanaandamana kulipwa madai yao.
Katika vurugu hizo polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni wanafunzi 86 wanaosoma program maalum ya Stashahada ya ualimu kwa tuhumuza za kuhamasisha uvunjifu wa amani na kufanya maandamano.
Wanafunzi hao waligoma kuingia darasani jana na kuamua kufanya maandamano ya amani kuelekea ofisi ya Waziri mkuu kwa lengo la kuwasilisha madai yao.
Wakati wakiandamana kwa kupitia njia za pembezoni kuelekea kwa Waziri Mkuu polisi walifika gafla na kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi na kushindwa kufika katika ofisi hizo.
Kamanda wa Polisi Dodoma David Misime alisema chanzo cha maandamano ni kutokana na makubaliano katika kikao chao wakidai kuomgezewa posho ya chakula na hata kiasi wanachopewa kinacheleweshwa bila sababu.
NIPASHE
Maofisa wawili wa Serikali Rugonzibwa Mujunangoma na Theophilo Bakwea wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya rushwa baada ya kudaiwa kupokea mgawo wa milioni485.1 kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyokua benki kuu ya Tanzania BoT walizohamishiwa na James Rugemarila.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka wa Taasis ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru, Leornad Swai akisaidiana na Max Ari ulidaiwa kuwa Februari 5 katika benki ya Mkombozi iliyopo Ilala Dar,mshtakiwa  huyo akiwa mkuu wa sheria wa Wizara hiyo alipokea rushwa.
Inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo alipmao licha ya kukana atakua nje kwa dhamana endapo atatimiza masharti kwa kujidhamini kwa fedha taslimu milioni 160 au hati ya mali isiyohamishika iliyo na thamani sawa na fedha hizo.
Katika kesi ya pilimjumbe wa kitengo cha kuidhinisha Tanesco kununua umeme wa IPTL katika Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Bakwea akiwa na cheo hicho alipokea rushwa ya milioni 161.7 kupitia kwenye akaunti yake toka kwa Rugemarila ikiwa ni mgawo wake kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.
NIPASHE
Wenyeviti wa Serikali  za vijiji 62 za vitongoji  294 vya Halmashauri ya Wilaya ya Hai wamegoma kuapishwa wakitaka ofisi ya ya Mkurugenzi huyo iwahakikishie watalipwa posho za nauli za chakula.
Tuio hilo lilitokea siku ya jumatatu na lilisimama zaidi ya saa tano kabla ya wenteviti hao kukubali kuendelea na zoezi la kuapishwa majira ya mchana baada ya kushaurinana nauongoziwa Halmashauri hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wenyeviti hao, walisema wanashangazwa na kitendo cha Halmashauri hiyo kushindwa kuwalipa posho za nauli,na chakula cha mchana.
Kutokana na mvutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Meleckzedeck Humbe, alitangaza kumsimamisha kazi kwa muda usiojulikana Mtendaji wa kata mpya ya Romu Khalifa Kwale kwa kushindwa kutimiza wajibu wake aliopewa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
MWANANCHI
Hofu imetanda kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya na Mikoa ya jirani baada ya kuzagaa kwa samaki wanaodaiwa kufa kwa sumu iliyotoka kwenye migoni ya nchi ya jirani ya Malawi kutokana na maji yake kutiririka kuelekea Ziwa Nyassa.
Taarifa za kuingizwa kwa samaki hao wanaodaiwa kuwa walikufa kwa sumu kwenye masoko mbalimbali Wilayani Kyela, Rungwe na Mbeya zilitolewa jana kwa mtandao na baadaye kutolewa tamko na viongozi wa Serikali.
Samaki hao wanadaiwa kuanza kufa tangu Januari 10 nchini Malawi na kwa upande wa Tanzania wameonekana tangu Januari 11 na kwamba hivi sasa wapo wanaoelekea majini kana kwamba wameanikwa.
Taarifa hiyo ilizua hamaki miongoni mwa wakazi ambapo Msaidizi mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro aliyetajwa kwa jina la Marco Masaya alipoulizwa kama wanayo taarifa ya kuzagaa kwa samaki hao alijibu kuwa ni kweli.
MWANANCHI
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa wa Masekelelo, wamefukia kaburi la Bernadetha Steven aliyezikwa na kifaranga cha kuku tumboni lililofukuliwa juzi na watu wasiojulikana kwa imani za kishirikina.
Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Shinyanga, Musa Talib alilaani kitendo cha kufukua kaburi la mwanamke huyo aliyefariki dunia tangu January 3 mwaka huu.
Talib alisema tukio hilo halivumiliki na aliwataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi ili kuwabaini watu hao waliohusika kufukua.
Mtu mwenye dini hawezi kufanya hivyo, hizi ni imani za kishirikina na haya mambo ndiyo yanafanya watu waende kwa waganga wa kienyeji, embu jiulize mtu ameshafariki, unakwenda kufukua kaburi unatafuta nini, naomba tushirikiane kuwakamata wahusika“alisema Talib.
MWANANCHI
Wazazi na walezi katika kijiji cha Katente Wilayani Bukombe, Mkoani Geita wamelazimika kuwarudisha watoto wao majumbani baada ya kushindwa kulipa ada ya shilingi 20,000 ili waweze kuanza darasa la kwanza katika shule ya msingi Mwenge.
Wazazi hao walisema wameambiwa fedha hizo ni kwa ajili ya kununua madawati pamoja na michango mingine.
“Kila mwaka nalipa mchango wa madawati, sasa kuna faida gani ya ulipia tena ? alihoji mmoja wa wazazi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo George Mahube alikiri watoto hao kurudishwa nyumbani kwa kukosa fedha ya madawati fedha za michango ya madawati, nembo ya shule na malipo ya walinzi.
MTANZANIA
Mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1500 wa Shirika la Reli Tanzania na Zambia TAZARA umeingia katika siku ya tatu leo huku uongozi wa Shirika hilo ukitoa wito kwa Serikali kuingilia kati.
Mkuu wa Kitengo cha mahusiano  Conrad Simuchile alisema wafanyakazi wa Shirika hilo wamekua wakilalamika mara kwa mara kutokana na shirika kuwa na uzalishaji mdogo unaozidi matumizi.
Matatizo ya Tazara hayajaanza leo, tatizo lililopo hapo si mshahara tu bali ni uzalishaji mdogo,Serikali za nchi zote mbili zinahitaji kutoa gedha au kutafuta mwekezaji ili kuiua Shirika, tunajiendesha kwa hasara kwa miaka kumi sasa,”alisema Simuchile.
Alisema ili kukidhi gharama za uendeshaji treni zinatakiwa kusafirisha tani 6,000,000 kwa mwaka lakini mpaka sasa zinabeba tani 2,000,000 tu.
TANZANIADAIMA
Wananchi wa kijiji cha Ijoka, Mkoani Mbeya wameingia kwenye imani za kishirikina baada ya kuandamana na kwenda kupasua mti ulianguka ambao wanadai una utajiri ndani yake.
Wakazi hao walisema walielezwa na mganga wa jadi kutoka Malawi Peter Lungola, kuwa mti huo ukitumiwa vyema utaleta utajiri.
Mganga huyo alifika kijiji humo miaka 20 iliyopitana kuwaeleza kuw amti huo  una asili kubwa ya utajiri na kuwa chini ya mti huo kuna nyumba za kifahari zilizojaa hazina kubwa ya fedha.
Inasemekana mti huo ulianguka wiki iliyopita na kuanza kupumua huku watu wakipata kiwewe huku nyoka mkubwa ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha.
Wazee wa kijiji hicho walishangazwa na hatua ya baadhi ya watu kula majani ya mti huo huku wengine wakichukua magome yake na kuyahifadhi majumbani mwao
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment