Hizi ni Story muhimu kwenye Magazeti ya leo Tanzania January 4,2015 Nimekuwekea hapa mtu wangu
MTANZANIA
Siku moja baada ya genge la uhalifu la Panya road kutekeleza vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam,siri ya mikakati ya kufanya mashambulizi na uendeshaji wa genge hilo sasa zimebainika.
Uchunguzi umebainika kuwa genge hilo linaongozwa na watu wenye utaalamu wa fani mbalimbali ambao kwa sababu ya kukosa ajira wamebaini mbinu ya kuendesha vitendo vya uhalifu ili kujipatia kipato.
Uchunguzi huo umeonyesha genge hilo linaloundwa na vijana wa shule ya Sekondari,makondakta wa magari ya abiria na vijana wasiokua na ajira na lina matawi karibu maeneo yote ya Dar es salaam.
Vijana wa kundi hilo wanaongozwa na makamanda wa vikosi vya maeneo yao na kupokea maelekezo ya kutekeleza uhalifu kutoka kwa kiongozi mkuu wa genge.
MTANZANIA
Magari yote yenye namba za usajili za Tanzania yanayofanya biashara ya kusafirisha abiria ikiwemo watalii kutoka Arusha kwenda Nairobi nchini Kenya yamezuiliwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Hatua ya kuyazuia magari hayo ilianza kuchukuliwa tangu Disemba 28 mwaka jana na mamlaka ya Serikali ya Kenya bila kueleza hasa Sababu za kuyazuia hayo kuingia uwanjani kama ilivyokua zamani.
Mmiliki wa kampuni ya Rainbow Shuttle Methew Molel alisema kitendo cha kuyazuia magari hayo na kusababisha kulipa gharama mara mbili ni hujuma kwa biashara yao.
“Tumesikitishwa na kitendo cha kuyazuia magari yetu umbali wa kilomita mbili hadi tatu kutoka uwanjani,ambapo tunalazimika kulipia tena ushuru kwa gharama ya dola 10 hadi 12 za Marekani kwa mgeni ,fedha ambayo ni karibu 22,000kwa fedha ya Kitanzania,hii ni hujuma kwa uchumi wa nchi yetu na ni dalili mbaya kwa mtangamano wa Jumuiya ya EAC”Alisema Mollel.
MTANZANIA
Watumishi mbalimbali wa Serikali wameumaliza vibaya mwaka 2014 baada ya kujikuta wakikatwa mara mbili madai ya mikopo yao kutokana na ucheleweshaji wa marejesho hayo kwenye benki.
Waziri wa fedha Saada Mkuya amesema tatizo hilo linatokana na mabadiliko ya mfumo wa utoaji wa mishahara yanayolenga kupambana na watumishi hewa.
Wafanyakazi wa chuo kikuu Huria cha Tanzania OUT wamesema kwa miezi mitatu mfululizo wamekua wakikatwa mara mbili malipo ya mikopo waliyochukua benki.
“Wafanyakazi wengi hapa tumekopa benki,tangu Oktiba mwaka jana tunakatwa mara mbili,afadhali sisi wahadhiri lakini kuna wafanyakazi wa chini wanakatwa mshahara wote wanabaki hawana kitu,unakuta mtu anapokea 40,000 kwa mwezi ataishije”alihoji mmoja wa wafanyazi hao wa OUT.
NIPASHE
Yale maelezo kuwa supu ya Pweza na dawa za mitishamba zinazotolewa na ‘Sangoma’ zinaongeza nguvu za kiume huenda yakawa si kweli baada ya kuwepo taarifa kuwa dawa hizo zinapunguza kama si kumaliza kabisa nguvu hizo.
Baadhi ya wateja na jamaa wanaotumia dawa hizo wamesema baadhi ya ndugu zao waliotumia dawa hizo wameshidwa kufanya tendo la ndoa.
Walisema wakati mwingine walivyoanza kuzitumia walipata uwezo wa kindoa lakini hali ilibadilika na nguvu ziliishi na sasa wanajuta kutumia dawa hizo.
Walidai kuwa waganga wa jadi na wapishi wa supu ya pweza wanawahadaa kuwa wanadawa lakini wanachotumia ni kuchanganya dawa zao na viagra.
Walisema kuna baadhi ya hotel na migahawa inasifika kwa kutengeneza dawa hizo zinazowavutia wateja na kushawishika kufunga safari kwenda kuzinunua lakini kinachoongezewa ni kusisimua misuli ya viungo ni tiba za kisasa na vingine vyote ni viini macho.
NIPASHE
Rais Jakaya Kikwete amemteua Naibu Mwanasheria mkuu George Masaju kuwa Mwanasheria mkuu wa Serikali kuchukua nafasi ya Fredrick Werema aliyejiuzulu.
Uteuzi wa Masaju ulianza ijumaa iliyopita na ataapishwa kesho ikulu kwa mujibu wa taarifa ya kurugenzi ya Mawasialino Ikulu.
Taarifa ilisema kabla ya uteuzi wake alikua Naibu Mwanasheria mkuu kadhalika alipata kuwa mshauri wa sheria wa Rais.
Uteuzi wa mwanasheria mpya unakuja wiki chache baada ya kujiuzulu kwa Jaji Werema aliyewajibika kutokana na ushbauri wake kwa Serikali na vyombo vingine vya utendaji kuhusuutoaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow kutolewa na kuleta mtafaruku.
MWANANCHI
Kamanda wa Polisi kanda ya Kinondoni Camilius Wambura alisema kuwa vijana watatu waliotoka Geita kuja Dar kwa lengo na kuonana na Rais na kukaidi amri ya kusitisha safari yao,wako nje kwa dhamana.
Kauli ya Wambura inatokana na vijana wa tatu kutoka Geita kutembea kwa miguu hadi Dar es salaam ili kuonana na Rais na kumweleza kero zao,ambapo walikamatwa baada ya kukaidi agizo la kusitisha safari yao.
Wambura alisema kinachofanyika kwa sasa ni taratibu za kusheria ikiwemo kufanyika kwa upelelezi na ukikamilika watawasiliana na mwanasheria wa Serikali kufahamu hatua gani inafuata.
Katibu mkuu wa Chadema Wilbroad Slaa alithibitisha mawakili wa chama hicho walikwenda kuwatoa vijana hao kwa maandishi na wamechukua jukumu la kuwasimamia mahakamani iwapo watashtakiwa.
MWANANCHI
Ahadi zilizotolewa na Rais Kikwete katika mikutano mbalimbali wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 huenda zikawa mwiba kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa sasa kutokana na nyingi kutotekelezwa au kuwa katika hatua za mwanzo.
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,kwa nyakati tofauti alitoa ahadi kuwasaidia kuwakwambua wananchi kutoka kwenye dimbwi la umaskini,maradhi na kuboresha upatikanaji wa elimu nchi,ahadi hizo zilitarajiw akupatikana kabla hajatoka madarakani.
Ikiwa imebaki takribani miezi 10 ya uongozi wa awamu ya pili kufikia ukomo,muda unakwenda haraka na utekelezaji wa ahadi hizo unasuasua jambo linalotia shaka iwapo kila ahadi itatekelezwa.
Kushindwa kutekelezwa kwa ahadi hizo ambazo zipo kwenye kitabu cha ahadi za Rais kilichoandaliwa na ofisi ya Waziri mkuu,kinaiweka Serikali ya CCM katika wakati mgumu hasa pale itakaporudi kwa wananchi kutoa ahadi nyingine kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ujao
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupiti, kumekucha blog
No comments:
Post a Comment