Huyu ndiye aliyeshinda Tuzo ya Golikipa Bora Ufaransa msimu wa 2013/2014
Golikipa Mnigeria Vincent Enyeama amechaguliwa kuwa kipa bora wa msimu uliopita kwenye ligi ya Ufaransa baada ya kuonyesha kiwango cha juu akiwa na timu yake ya Lille Metropole katika msimu wa mwaka 2013/ 2014.
Enyeama alifanya vizuri akiwa na timu hiyo ambapo alicheza kwenye mechi 20 kati ya 56 ambazo hakuruhusu kufungwa bao hata moja.
Golikipa huyo ambaye pia ni nahodha wa
timu ya taifa ya Nigeria anatwaa tuzo hii kwa msimu wake wa pili
mfululizo baada ya kuitwaa tena katika msimu wa miaka 2012/2013 baada ya
kurudi kwenye klabu hiyo akitokea klabu ya Macabbi Haifa ya Israel ambako alikwenda kucheza kwa mkopo.
Mwaka 2014 ulikuwa mwaka wa mafanikio kwa Enyeama
baada ya kipa huyo kuonyesha kiwango cha juu kwenye michuano ya kombe
la dunia akiwa na timu na taifa ya Nigeria ambayo aliiongoza kufuzu
hatua ya 16 ya michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.
Kipa huyu pia ameingia kwenye
kinyang’anyiro cha tuzo za mwanasoka bora barani Afrika ambako ameingia
fainali akiwa na kiungo wa Ivory Coast, Yaya Toure na mshambuliaji wa Gabon, Pierre Aubameyang.
No comments:
Post a Comment