Tangakumekuchablog
Tanga,POLISI Mkoani Tanga inawashikilia
watu watatu wakazi wa Kigamboni Dar es Salaam kwa tuhuma za kusafirisha
mihadharati aina ya mirungi viroba 18 walivyovificha katika shehena ya mbao
zikisafirishwa kuelekea Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu kamanda wa polisi Mkoani
Tanga, Juma Ndaki alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10 za usiku katika
kizuizi cha polisi kijiji cha Chekelei barabara ielekeayo Mombo, Segera.
Aliwataja
watu hao kuwa ni Sara Mbwambo(38), Robison Sam(24) na Godfrey Machumbe (30)
wote wakiwa ni wakazi wa Dar es Salaam Wilaya ya Kinondoni.
Alisema viroba
hivyo vilifichwa katikati ya mbao jambo ambalo haikuwa rahisi kugundua na
polisi walitilia shaka baada ya kusikia harufu ambayo si ya kawaida na kudhani
kuna kitu kifananacho na madawa ya kulevya.
“Unajua sasa
hivi kuna kila aina ya mbinu zinazotumika kusafirisha madawa ya
kulevya----mbinu hizo nasi tunazijua na ndio maana kila wanavyofanya
tunawagundua” alisema Ndaki
“Katika kila
kizuizi cha polisi tumeweka wataalamu wa kubaini madawa ya kulevya na ndio
tumefanikiwa hakuna anaepita hata kama ameficha ndani ya tairi na kuweka upepo
tutagundua” alisema
Katika tukio
jengine Ndaki alilitaja kuwa polisi inamtafuta mkazi wa Lushoto, Farid Jumaa
kwa tuhuma za kusafirisha bangi kilo 64 na kuficha katika magunia ya vitunguu
maji.
Alisema
tukio hilo lilitokea juzi saa 1 jioni katika kizuizi cha polisi cha Mombo
wakati akisafirisha kuelekea Mkoa wa
Kilimanjaro na kupakia katika gari dogo ya matumizi ya nyumbani.
“Tulipoisimamisha
gari jambo la kwanza tulisikia harufu kali ambayo sio ya kawaida na kuacha hata ukaguzi wa gari----kwanza
tulitaka kuteremsha magunia ambayo yalikuwa kwenye buti” alisema Ndaki
“Dereva
aligoma kuyashusha na kudai ni vitunguu maji na nyanya ikiwa ni zawadi ya
kupeleka kwa wazazi Machame Kilimanjaro---tuliyashusha kwa nguvu na kuyapasua
na kila gunia kulikuwa na roba la bangi” alisema
Kamanda
Ndaki aliwataka wadereva kuacha kuchukua mizigo ambayo hawana uhakika nayo na
hivyo kuwashauri wahakikishe mzigo wanaobeba watautambua na kuwa tayari
kuutolea maelezo ili kuepusha kuingia katika matatizo.
No comments:
Post a Comment