Wednesday, August 31, 2016
JACK WILSHERE HATIMAE ATIMKIA BOURNEMOUTH
Jack Wilshere kujiunga na Bournemouth
Kiungo wa kati wa
Arsenal Jack Wilshere anakaribia kujiunga na klabu ya Bournemouth kwa
mkopo wa muda wa msimu uliosalia baada ya mpango wa kuijiunga na klabu
ya Roma kuzuiwa na Arsenal.
The Gunners ilikataa kufanya biashara
na Roma kwa sababu ya vile walivyochukulia uhamisho wa beki Kostas
Manolas mapema msimu huu.Wilshere mwenye umri wa miaka 24 alifanya mazungumzo na Bournemouth na Crystal Palace.
Anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu na The Cherries.
JOHN KERRY AKUMBANA NA FOLENI NEW DELH
John Kerry akwama kwenye foleni Delhi, India
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alipofika Delhi kwa mashauriano na maafisa wa serikali Jumatatu jioni, hakuwa na bahati.Mvua kubwa ilinyesha na 'kukosa kutambua cheo chake'.
Badala ya magari yake kupitia barabara zilizo wazi, msafara wake wa magari ulikwama kwenye foleni zaidi ya saa moja.
Lilikuwa jambo lisilo la kawaida kwa sababu maafisa wa usalama huondoa magari barabarani kutengeneza njia ya kutumiwa na wageni mashuhuri.
BARABARA YA KOROGWE ROAD ENEO LA KWAFUNGO MUHEZA
Gari aina ya Carry ikiwa imepakiza abiria
kupitiliza wakipandisha mlima wa Kwafungo
Muheza Tanga na mbele yao waendesha bodaboda wakiendesha pikipiki wakiwa
hawana kofia ngumu ya kichwani.
UKUTA WAAHIRISHA MAANDAMANO KESHO
Upinzani waahirisha maandamano
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho.
Viongozi wa upinzani, akiwemo Edward Lowassa wa Chadema, wametangaza hatua hiyo kwenye kikao na wanahabari Dar es Salaam.Wamesema wameahirisha maandamano hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kusikia ombi la viongozi wa kidini na wadau wengine waliowaomba kukumbatia na kuyapa muda mazungumzo.
Viongozi wa chama hicho walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa Septemba Mosi kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na serikali.
Baada ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi walisema: "Yapo Matukio ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza demokrasia na misingi ikipuuzwa na kudharauliwa.
"Si nia ya Chadema kugombana na Serikali bali ni kazi ya Chama Pinzani kuisaidia Serikali iongoze kwa kufuata misingi ya Katiba," chama hicho kilisema.
Maandamano hayo yalipewa jina Ukuta, ikisimamia Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania.
Serikali ilipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa, ya hadhara na ya ukumbini. Baadhi ya viongozi wa upinzani wamekamatwa na kuzuiliwa kwa muda.
MKUU WA WILAYA HANDENI GODWEN GONDWE AWATAKA WAKULIMA KULITUMIA SOKO LA (EAC)
Tangakumekuchablog
Mkulima wa machungwa Kabuku Handeni Tanga, Rajab Lusewa akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
Mkulima wa machungwa Kabuku Handeni Tanga, Bakari Mgaza, akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
Mkulima wa machungwa Kabuku Wilayani Handeni Tanga, Said Msagati akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
Handeni, MKUU wa
Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, amewataka wakulima wa machungwa Wilayani humo
kutafuta masoko nje likiwmo soko la pamoja la Afrika Mashariki (EAC) kuepuka
kulanguliwa na walanguzi wanaowafuata mashambani.
Akizungumza katika kikao mara baada
ya kukabidhiwa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) kwa
halmashauri ya Wilaya hiyo jana, Gondwe alisema wakulima wa machungwa wanashindwa kuwa wakulima wa kisasa baada
kushindwa kuthubutu kutafuta masoko nje.
Alisema soko la pamoja na Jumuiya ya
Afrika Mashariki lipo lakini wanashindwa kulitumia badala yake wafanyabiashara
wa nje huja mashambani kwao na kuwalangua kwa bei ya hasara.
“Kila mtu ndani na nje ya nchi
wanajua kuwa Handeni inalima kilimo cha cha machungwa kwa wingi na
wafanyabiashara huja , ila niwaambieni kuwa munalanguliwa kwa woga wa kwenda
kutafuta masoko ” alisema Gondwe na kuongeza
“Soko la pamoja lipo wazi bila
vikwazo vyoyote sasa ni kitu gani kinachotufanya kushindwa kulitumia na
kuwaachia wenzetu kuja kwetu na kutulangua kwa bei ya kutupa hebu jamani
tuondoe woga na tuwe tayari” alisema
Aliwataka wakulima kuacha woga na
badala yake kuwa tayari kutafuta masoko ndani na nje ya nchi na kuwa wakulima
wakubwa na kuacha kulanguliwa na wafanyabiashara mashambani ilhali fursa zipo.
Akizungumza katika kikao hicho
Mwenyekiti wa Wafanyabiasha wa Machungwa Segera, Hussein Diamballa, aliwataka
wafanyabiashara hao kucha kuuza machungwa yaliyopepewa na kusema kuwa kufanya hivyo
kunaondosha sifa ya machungwa kituoni hapo.
Alisema kuna wachuuzi ambao wamekuwa
wakiuza machungwa yaliyopepewa na kuchanganya mabovu na hivyo kuwataka kuacha
kufanya hivyo kwani watafanya ukaguzi wa mtu mmoja mmoja.
Alisema umoja huo uko mbioni
kusajili wanachama ambao utakuwa na utaratibu wa kutoa namba na sare hivyo
kuwataka kufanya biashara ya halali na kuacha udanyanyifu.
“Tunataka kuondosha ile dhana ya
kituo chetu kuuza machungwa ya kupepea na kubambika mabovu, hii inatuletea sifa
mbaya wakati hapa tunalima machungwa mazuri yenye maji mengi” alisema Diambala
Aliwataka wafanyabiashara hao
kuwafichua wachuuzi wenye kufanya udanganyifu na kuwaletea sifa m,baya kwa
wateja ilhali kituo hicho ni muunganisho wa magari yaendayo Mikoani jambo
ambalo linaweza kuuza na kupata mitaji na kuwa wafanyabiashara wakubwa.
Mwisho
Wakulima wa machungwa Kabuku
Wilayani Handeni Tanga wakiwa katika semina ya kilimo cha machungwa na halizeti
wakati wa kujadili andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho
Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
.
Mkulima wa machungwa Kabuku Handeni Tanga, Rajab Lusewa akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
Mkulima wa machungwa Kabuku Handeni Tanga, Bakari Mgaza, akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
Mkulima wa machungwa Kabuku Wilayani Handeni Tanga, Said Msagati akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
Subscribe to:
Posts (Atom)