Ibada yafanyika kwa ajili ya waliokufa katika tetemeko la ardhi
Ibada ya wafu imefanyika
nchini Italia kwa ajili ya watu 290 waliofariki dunia katika tetemeko
kubwa lililoikumba nchi hiyo siku ya Jumatano wiki hii.
Siku ya
kitaifa ya maombolezi imeanza nchini Italia, kuwaomboleza waathiriwa wa
tetemeko kubwa la ardhi, lilokumba maeneo ya katikati mwa taifa hilo.Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi amehudhuria mazishi ya mazishi ya kitaifa ya waliofariki dunia katika eneo lililopata pigo kubwa, Arquata.
Zaidi ya watu 280 wanaaminika kwamba wameaga dunia.
Takriban watu 400 kwa sasa wanatibiwa hospitalini.
Matumaini ya kupata watu wakiwa hai kwenye vifusi vya majengo yaliyobomolewa yanafifia baada ya siku tatu za uokoaji.
Raia wengi wa Italia waliaga dunia, pamoja na raia kadhaa wa kigeni.
No comments:
Post a Comment