Abeba maiti ya mkewe 12km
Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alifariki dunia baada ya kuugua maradhi ya kifua kikuu katika hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa.
Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilimita 60 na hakuwa na uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kuwabebea wagonjwa.
Hospitali hiyo imekana madai hayo.
'Hakuna namna'
'Mwanamke huyo alilazwa hospitalini siku ya Jumanne na kufariki usiku huo huo.alichukua maiti hiyo bila kuwafahamisha wahudumu wa hospitali hiyo,' afisa mkuu wa afya B Brahma alisema
Bwana Majhi, anadai mkewe alifariki siku ya Juma nne usiku na kuamua kubeba mwili wake siku ya Jumatano baada ya wahudumu wa hospitali hiyo kumsihi kuondoa mwili huo.
Alitembea kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na kumsaidia kwa gari la kubebea wagonjwa wakamfikisha hadi mwisho wa safari yake.
Shughuli ya kuchoma mwili wa mkewe ilifanyika siku ya Jumatano usiku.
BBC
No comments:
Post a Comment