Tangakumekuchablog
Handeni, WAZIRI
wa Nishati na Madini, Sospeter Mohongo, amewataka wakulima wa mbogamboga na
matunda vijijini kuitumia fursa ya ujio wa umeme vijijini wa Rea kwa kufungua
miradi na viwanda vidogovidogo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini (TREEP) awamu ya pili kijiji cha
Kwedizinga kata ya Kabuku Wilayani Handeni kwa ufadhili wa Benki ya Dunia,
Muhongo alisema Serikali inataka kila mwananchi kutumia nishati ya umeme
majumbani.
Alisema wananchi vijijini wako na
fursa nyingi za maendeleo laikini wamekuwa duni kutokana nna kutokuwa na
nishati ya umeme hivyo kuwataka kuhakikisha wanafunga umeme majumbani kwao.
“Hapana shaka kuwa wananchi wa
vijijini ni matajiri lakini utajiri wao hauonekani na badala yake wenye pesa
huwatishia mazao yao kununua kwa bei ya hasara kutokana na kutokuwa na umeme”
alisema Muhongo na kuongeza
“Mahindi na mpunga wenu mutakoboa
hapa hapa na sio tena mjini, wanunuzi watakuja kwenu na kuwauzia kwa bei
munayotaka nyinyi tofauti na sasa ambapo hamuna umeme na kulazimika kuwauzia
kwa bei ya hasara” alisema
Aliwaka wananchi hao kuhakikisha
awamu ya pili ya usambazaji umeme vijijini wananchi haiwapiti hivyo kutaka
wenye mifugo na rasilimali yoyote kuuza na kupata pesa za kulipia umeme huo.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Bank
ya Dunia, Bella Bard, alisema anajua umuhimu wa nishati ya umeme majumbani na
kuona ili kuondosha umasikini ;lazima umeme uwepo.
Alisema Bank ya Dunia inatambua kuwa
vijijini ziko fursa nyingi za maendeleo lakini kikwazo kikubwa ni umeme hivyo
kwa ujio huo nikuwataka kila mmoja anakamilisha taratibu za kufungiwa.
“Tunatambua kuwa umasikini uko mjini
na sio vijijini ambako umasikini wao ni kutokana na kutokuwa na umeme tu, hii
kwa kweli ni changamoto ambayo tumeigundua
na ndio maana nguvu za Serikali na bank ya dunia imejikita kusambaza vijijini”
alisema Bard
Aliwataka wananchi waishio karibu na
nyya za umeme ulipopita kuhakikisha inailinda miundombinu yake pamoja na kuzuia
hujuma yoyote ambayo itaathiri mradi huo wa usambazaji umeme vijijini
Mwisho
Waziri wa Nishati na Madini, Sosper Muhongo akikata uzi kuzindua mradi Kabambe wa kusambaza Umeme Vijijini (TREEP) kijiji cha Kwedizinga kata ya Kabuku Wilayani Handeni Mkoani Tanga, kushoto kwake ni Mwakilishi wa Baenk ya Dunai, Bella Bird. wanzo kulia ni Gabriel Robart na kushoto mwisho ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella
,Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mohongo (kushoto) na Mwakilishi wa Bank ya Dunia , Bella Bird (kushoto) wakizindua Mradi Kabambe wa kusambaza Umeme Vijijini (TREEP) kijiji cha Kwedizinga kata ya Kabuku Wilayani Handeni
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment