Misri imepitisha sheria kali dhidi ya Ukeketaji
Mamlaka nchini
Misri imeongeza adhabu kwa yeyote atakae walazimisha watoto wa kike
kukeketwa. Sheria imependekeza kifungo gerezani kati ya miezi mitatu
hadi miaka mitatu kwa mtu atakaepatikana na hatia.Huku baraza la
mawaziri limepitisha mpango wa kifungo cha gerezani kati ya miaka mitano
hadi saba.
Hukumu ya miaka kumi na mitano inaweza kutumika pale
ambapo kitendo hicho cha ukeketaji kitasababisha ulemavu. Ukeketaji
umekuwa ni suala lisilokubalika kisheria nchini misri tangu mwaka 2008
lakini vitendo hivyo vya ukeketaji vimekuwa vikienea kila uchao nchini
humo.BBC
No comments:
Post a Comment