Mkuu wa FIFA wa zamani Sepp Blatter mahakamani tena
.Blatter anahudhuria mahakamani kusikiliza kesi hiyo inayoendeshwa na mahakama ya usuluhishi wa mizozo michezoni nchini Uswizi.
Akizungumza na maripota mjini Lausanne, amejielezea kama mtu mwenye matumaini.
Blatter aliwekewa marufuku hiyo mwezi Disemba mwaka jana kwasababu aliidhinisha malipo ya zaidi ya dola milioni mbili kwa mkuu wa zamani wa soka barani Ulaya , Michel Platini, miaka mitano iliyopita.
Mwezi Mei, Platini alishindwa kushawishi kuondolewa kwa marufuku dhidi yake, ingawa ilipunguzwa kutoka miaka sita hadi miaka minne.
No comments:
Post a Comment