Tangakumekuchablog
Lushoto, WAZIRI
wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, amelitaka shirika la Umeme Tanzania
Tanesco Mkoa wa Tanga, kutoa elimu kwa wananchi vijijini juu ya umuhimu wa
kuunganishwa umeme wa mradi wa Rea.
Akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara leo Wilayani hapa, Muhongo alisema kuna muitikio mdogo wa wananchi vijijini
waliojitokeza kuomba umeme tofauti na malengo yaliyokusudiwa.
Alisema kuna baadhi ya maeneo yenye
kaya zaidi ya 300 watu waliojitokeza kuomba umeme hawazidi 100 hivyo upo umuhimu wa shirika hilo
kufanya mikutano ya wananchi vijijini kutoa elimu ya umeme wa Rea.
“Tumepita maeneo mbalimbali na
wananchi kusema hawajui wapi wananzia na nani wanamuona kuchukua fomu ya
maombi, hivyo ni dhahiri kuwa kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi” alisema
Muhongo na kuongeza
“Niwatake nyinyi tanesco kuhakikisha
awamu hii ya pili ya usambazaji umeme vijijini inafikia malengo ili tukienda
awamu ya tatu tuwe tumevuka malengo tuliyojiwekea” alisema
Profesa Muhongo aliwataka wananchi
kuhakikisha fursa hiyo ya usambazaji umeme vijijini awamu ya pili wanaitumia
ikiwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kila kaya mjini na vijijini anatumia
nishati ya umeme.
Alisema ujio wa umeme huo ni fursa
pekee ya kuongeza kipato cha mwananchi wakiwemo wakulima badala ya kwenda mjini
kukoboa mahindi na kusindika matunda shughuli zote zinafanyika vijijini.
Alisema badala ya wawekezaji kujenga
viwanda vya kusindika matunda na mbogamboga mjini wanaweza kuwafuata wakulima mashambani na kuweza kupata unafuu na
kuboresha kilimo chao na kuwa wakulima wa kisasa.
Kwa upande wake Meneja wa Tanesco
Mkoa wa Tanga, Abrahman Nyenye
alisema shirika hilo limekuwa karibu na wananchi pamoja na viongozi wa
vitongoji na vijiji juu ya mradi wa usambazaji umeme vijijini .
Alisema muitiko wa wananchi ni
mkubwa lakini kuna baadhi ya nyumba hazikidhi haja ya kufungiwa umeme kutokana
na kuwa za nyasi hivyo kutoa elimu ya kuboresha numba zao na kuweza kupata
umeme.
Alisema nyumba za nyasi Shirika hilo
la Tanesco limekuwa likitoa maelekeo na elimu kuwataka kuboresha nyumba zao
kwanza ili kuweza kupata kufungiwa umeme na kusema wengi wamekuwa wakifanya
marekebisho.
Mwisho
Wazee wa Mlola Wilayani Lushoto
Mkoani Tanga, Abeid Othman (kushoto) , Rajab Saguti (kulia) wakimpa salamu
Waziri wa Nishati na Madini , Sospeter Muhongo (katikati) kufikisha kilio
cha kwa Rais wa John Pombe Magufuli kuwa
toka Uhuru hakuna Rais yoyote aliewahi kufika jimboni humo hivyo kumtaka
kuwatembelea.
No comments:
Post a Comment