Handeni, MKUU wa
Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, amewataka wakulima wa machungwa Wilayani humo
kutafuta masoko nje likiwmo soko la pamoja la Afrika Mashariki (EAC) kuepuka
kulanguliwa na walanguzi wanaowafuata mashambani.
Akizungumza katika kikao mara baada
ya kukabidhiwa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) kwa
halmashauri ya Wilaya hiyo jana, Gondwe alisema wakulima wa machungwa wanashindwa kuwa wakulima wa kisasa baada
kushindwa kuthubutu kutafuta masoko nje.
Alisema soko la pamoja na Jumuiya ya
Afrika Mashariki lipo lakini wanashindwa kulitumia badala yake wafanyabiashara
wa nje huja mashambani kwao na kuwalangua kwa bei ya hasara.
“Kila mtu ndani na nje ya nchi
wanajua kuwa Handeni inalima kilimo cha cha machungwa kwa wingi na
wafanyabiashara huja , ila niwaambieni kuwa munalanguliwa kwa woga wa kwenda
kutafuta masoko ” alisema Gondwe na kuongeza
“Soko la pamoja lipo wazi bila
vikwazo vyoyote sasa ni kitu gani kinachotufanya kushindwa kulitumia na
kuwaachia wenzetu kuja kwetu na kutulangua kwa bei ya kutupa hebu jamani
tuondoe woga na tuwe tayari” alisema
Aliwataka wakulima kuacha woga na
badala yake kuwa tayari kutafuta masoko ndani na nje ya nchi na kuwa wakulima
wakubwa na kuacha kulanguliwa na wafanyabiashara mashambani ilhali fursa zipo.
Akizungumza katika kikao hicho
Mwenyekiti wa Wafanyabiasha wa Machungwa Segera, Hussein Diamballa, aliwataka
wafanyabiashara hao kucha kuuza machungwa yaliyopepewa na kusema kuwa kufanya hivyo
kunaondosha sifa ya machungwa kituoni hapo.
Alisema kuna wachuuzi ambao wamekuwa
wakiuza machungwa yaliyopepewa na kuchanganya mabovu na hivyo kuwataka kuacha
kufanya hivyo kwani watafanya ukaguzi wa mtu mmoja mmoja.
Alisema umoja huo uko mbioni
kusajili wanachama ambao utakuwa na utaratibu wa kutoa namba na sare hivyo
kuwataka kufanya biashara ya halali na kuacha udanyanyifu.
“Tunataka kuondosha ile dhana ya
kituo chetu kuuza machungwa ya kupepea na kubambika mabovu, hii inatuletea sifa
mbaya wakati hapa tunalima machungwa mazuri yenye maji mengi” alisema Diambala
Aliwataka wafanyabiashara hao
kuwafichua wachuuzi wenye kufanya udanganyifu na kuwaletea sifa m,baya kwa
wateja ilhali kituo hicho ni muunganisho wa magari yaendayo Mikoani jambo
ambalo linaweza kuuza na kupata mitaji na kuwa wafanyabiashara wakubwa.
Mwisho
Wakulima wa machungwa Kabuku
Wilayani Handeni Tanga wakiwa katika semina ya kilimo cha machungwa na halizeti
wakati wa kujadili andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho
Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
.
Mkulima wa machungwa Kabuku Handeni Tanga, Rajab Lusewa akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
Mkulima wa machungwa Kabuku Handeni Tanga, Bakari Mgaza, akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
Mkulima wa machungwa Kabuku Wilayani Handeni Tanga, Said Msagati akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
No comments:
Post a Comment