Tangakumekuchablog
Handeni, WAKAZI
wa Misima, Sindeni na Kwamatuku Wilayani
Handeni Mkoani Tanga, wamelalamika kero ya maji na kumuomba Waziri wa Maji
kuimaliza kero hiyo ambayo imedumu kwa miaka mingi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na
Mwandishi wa habari hizi jana, wakazi hao wamesema wamekuwa wakitumia maji mito
na madimbwi kwa matumizi ya nyumbani jambo ambalo linahatarisha usalama wa afya
zao.
Walisema maji hayo ambayo hutumiwa
na mifugo kwa kunyweshea wamedai kuwa
mara nyingi hupatwa na magonjwa ya kichocho na kuugua matumbo jambo ambalo ni hatari.
“Hapa kilio chetu kikubwa ni kero ya maji na kwa sasa tunatumia ya
madimbwi ambayo hutumiwa pia na mifugo, hii ni hatari na ndio mara nyingi
tunaugua magonjwa ya matumbo na kichocho” alisema Saiomon Mkokoi
“Kero hii imedumu miaka mingi
hatujui tatizo liko wapi wakati mji wetu uko na ardhi yenye rutuba nzuri,
basituchimbiwe kisima kimoja tu na kuwa na uhakika wa maji safi ili kuepukana
na kununua maji kila siku “ alisema Mkokoi
Alisema kwa sasa kilio chao
wanakipeleka kwa Waziri wa maji kwa
imani kuwa
ndio kimbilio pekee na mkombozi baada ya jitihada za viongozi waliopita
kushindwa
Kwa upande wake mfugaji jamii ya kimasai mkazi wa Sindeni Olengusa
Papai, alisema mara nyingi huingia ugomvi wa wananchi juu ya matumizi ya maji
ya mabwawa ambayo huwa ni yakunyeshea mifugo.
Alisema ugomvi huo unakuja kutokana
na maji hayo kutumika kwa matumizi ya binadamu na mifugo hivyo huwa na wakati mgumu
kutokana na mabwawa hayo kuwa machache.
“Kila siku sisi wafugaji na wananchi
tumekuwa tukiingia katika ugomvi juu ya matumizi ya mabwawa, ni kweli kero ya
maji ni kubwa lakini hakuna mbadala maji haya haya ni matumizi ya binadamu na
mifugo” alisema
Alisema awali kulikuwa na utaratibu
wa matumizi ya mabwawa ambapo ya mifugo lilitengwa peke yake lakini shida
inakuja wakati wa kiangazi ambapo madimbwi mengi hukauka na kila mmoja
kukimbilia lililo na maji.
Mwisho
No comments:
Post a Comment