Wapenzi wa kichina wafunga ndoa kwenye daraja la kioo juu ya bonde
Si jambo linaloweza
kufikiriwa na kila mtu kulitenda wakati wa siku maalum, Lakini wapenzi
wa kichina walichagua kusherehekea harusi yao huku wakielea angani
katika daraja la kioo.
Bibi harusi na bwana harusi walioana katika
daraja la Shiniuzhai katika mji wa Pingjiang jimbo la Hunan katika
siku ya wapendanao ya uchina inayoadhimishwa tarehe 9 Agosti, Shirika la
habari la China News Service limeripoti.
Licha ya kuelea angani
yapata futi 590 kutoka usawa wa ardhi , waliweza kuonyesha tabasamu zao
walipokuwa wakipigwa picha za harusi yao.
Madaraja ya vioo yamekuwa maarufu sana nchini uchina hivi karibuni. Wiki chache tu zilizopita , maharusi wengine
waliamua kuvalishana pete kwenye daraja hilo hili ingawa hawakutoka
kwenye daraja
No comments:
Post a Comment