Wednesday, August 24, 2016

DEGE KUBWA ZAIDI DUNIA LAANGUKA

Ndege ndefu zaidi duniani - Airlander 10 - imeharibika baada ya kuanguka ikitua kwenye safari yake ya pili ya kufanyiwa majaribio.
Ndege hiyo ya urefu wa 302ft (92m) - ambayo kwa kiasi fulani ni ndege na pia kwa kiasi fulani puto - iliharibika ikiwa katika uwanja wa Cardington, Bedfordshire nchini Uingereza.
Ndege hiyo ya thamani ya £25m imeharibika eneo wanamoketi marubani baada ya kuangika kwa 'pua' mwendo wa saa tano saa za Uingereza.
  • Airlander
Airlander 10AirlanderMsemaji wa HAV, kampuni iliyounda ndege hiyo, amesema marubani na wahudumu wengine wote wako salama.
Kampuni hiyo imekanusha madai kwamba waya uliokuwa umening'inia kutoka kwenye ndege hiyo ulikwama kwenye kigingi cha nyaya za simu na kusababisha ajali hiyo.
Ndege hiyo ilifanya safari yake ya kwanza 17 Agosti.

No comments:

Post a Comment