Tangakumekuchablog
Mlalo, WAZIRI
wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, amesema Serikali imeadhimia usambazaji
umeme vijijini (Rea) kuhakikisha shule, hospitali na vituo vya afya vinakuwa na
umeme lengo likiwa ni kuondosha kero na kuongeza ufanisi.
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara jana, Muhongo alisema Serikali inatambua kero ya wanafunzi kukosa
huduma ya umeme pamoja na vituo vya afya hasa nyakati z ausiku.
Alisema shule zote za mjini na
vijijini pamoja na zahanati ifikapo mwaka 2020 ziwe zinatumia umeme na
kuondokana na kutumia mishumaa jambo ambalo ni hatari kiafya na usalama.
“Serikali haitaki kuona wanafunzi
wanatumia mishumaa kujisomea usiku, vilevile pamoja a vituo vya zahanati
madaktari na manesi kutumia tochi mfumo huo uwe mwisho” alisema M,uhongo na
kuongeza
“Kama umeme umeshafika hadi vijijini
kuna sababu gani shule na vituo vya afya visiwe na umeme ilhali nguzo zinapita
juu ya majengo yao” alisema
Akizungumza katika muktano huo,
Mbunge wa jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) Mkoa wa Tanga kuwaekea ofisi ya kupokea taarifa na malalamiko katika kila
jimbo ya majimbo ya Lushoto.
Alisema kwa sasa wateja wa umeme
wamekuwa wakisafiri zaidi ya kilometa 80 kwenda Lushoto kupata huduma ya umeme
jambo ambalo wananchi limewachosha hivyo kutaka kuangalia kwa jicho la pili.
Alisema kuwepo kwa umeme mashuleni
kutaweza kuwa msaada kwa wanafunzi kujisomea ikiwa na pamoja na kuongeza uelewa
pampja na kuondosha alama sifuri shule.
Mwisho
Kwa habari, matukio na michezo ni hap[ahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment