Tangakumekuchablog
Pangani,WAZIRI wa
Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, ametoa agizo Tanesco Makao Makuu , Mikoani
na Wilayani kutoa elimu nyumba kwa
nyumba ili ifikapo mwaka 2020 kila
nyumba inatumia nishati ya umeme.
Agizo hilo limekuja baada ya
wananchi katika ziara yake ya kutembelea miradi ya usambazaji umeme Rea nchini
kusema hawana elimu ya kutosha ya umeme wa
Rea .
Alisema Serikali imejiwekea malengo
ifikapo mwaka 2020 kila Mtanzania anatumia umeme na Serikali kuuza nje ya nchi hivyo
kuwataka Tansco kutoa elimu nyumba kwa nyumba lengo likiwa ni kupata elimu ya
kutosha ya umeme wa Rea.
“Ndugu zangu natambua kuwa nyinyi ni
wakulima wazuri wa mbogamboga na matunda
hapa kijijini, ushauri wangu awamu hii
ya usambazaji umeme vijijini awamu ya pili usiwapite kwani gharama zake ziko
chini kabisa” alisema Muhongo na kuongeza
“Nyanya na mapapai pamoja na
machungwa nitafurahi kuona miongoni
mwenu anawekeza kwa kufungua kiwanda cha kusindika matunda na wakulima kuwa na soko la uhakika la kuuzia
mazao yao” alisema
Aliwataka wananchi kuhakikisha awamu hii ya pili wa usambazaji umeme vijijini haupiti hivyo
kila mmoja kutambua kuwa umeme ndio msingi wa maendeleo ya maisha ya kila mtu.
Akizungumza katika mkutano huo,
Mbunge wa jimbo la Pangani Jumaa Awesso, amewataka wananchi kuitumia fursa hiyo
ya kupata umeme wa Rea ili kuongeza kipato.
Alisema ujio wa umeme huo utaweza
kuwavuta wawekezaji hasa eneo la Mkalamo ambalo liko na madini hivyo kusema kuwa fursa za maendeleo
ziko nyingi mara baada ya kuingia majumbani.
Aliwataka wananchi hao kuhakikisha fursa ya ujio wa umeme wa gharama
nafuu haupiti na kuweza kufanya jitihada kwani baada ya hapo gharama
za kufungiwa umeme zitakuwa juu na kuwa
vigumu kwa mwananchi wa kipato cha chini kumudu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment