Wanafunzi kuingia na bunduki darasani Texas, Marekani
Wanafunzi wa vyuo katika jimbo la Texas, Marekani wameruhusiwa kuingia na bunduki darasani.
Hii
ni baada ya maprofesa wawili kushindwa kwenye ombi lao la kutaka
mahakama izuiwe kutekelezwa kwa sheria mpya inayowaruhusu wanafunzi
kubeba bunduki bila kuzionyesha hadharani.Jaji katika mji wa Austin alipuuzilia mbali madai ya wahadhiri hao kwamba kuwepo kwa bunduki huenda kukawa hatari kubwa iwapo mjadala mkali utazuka darasani.
Mwanasheria mkuu wa Texas, Ken Paxton, ambaye ni wa chama cha Republican, aliunga mkono uamuzi wa jaji.
Alisema raia wanaotii sheria wana haki ya kujilinda hata wakiwa kwenye vyuo vikuu.
Jimbo la Texas lilipitisha sheria ya kuwaruhusu raia kubeba bunduki bila kuzionyesha hadharani miaka 20 iliyopita ingawa watu hawakuruhusiwa kuingia nazo vyuoni.
Hilo lilibadilishwa wiki tatu zilizopita kupitia marekebisho ya sheria.
No comments:
Post a Comment