Daraja refu zaidi la kioo kufunguliwa China
Daraja refu zaidi
duniani ambalo sakafu yake ni kioo litafunguliwa katika mji wa
Zhangjiajie katika
Daraja
hilo ndilo la juu zaidi lenye sakafu ya kioo duniani na linaunganisha
milima miwili ambayo hufahamika kama Milima ya Avatar. Filamu ya Avatar
iliandaliwa katika milima hiyo.Ujenzi ulikamilika Desemba mwaka jana. Urefu wa daraja hilo ni 430m na liligharimu $3.4m (£2.6m).
Daraja hilo limewekwa 300m juu ya ardhi, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la Xinhua.
Sakafu yake imeundwa kwa vipande 90 vya vioo ambavyo vina tabaka tatu.
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, daraja hilo lenye upana wa mita 6, ambalo mchoro wake uliandaliwa na msanifu mijengo kutoka Israel Haim Dotan, tayari limeweka rekodi kadha za dunia katika usanifu mijengo na ujenzi.
No comments:
Post a Comment