Tangakumekuchablog
Tanga, MTOTO wa miaka 6 Mwanaisha Athumani na Balizahu Juma (50) wote
wakazi wa Manolo tarafa ya Mlalo
Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, wamefariki dunia na wengie wanne kujeruhiwa
baada ya nyumba yao kuungua moto wakati wakiwa wamelala.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Leo, kamanda wa polisi Tanga, Benedickt
Wakulyamba, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2; 30 usiku wakati
wakijiandaa kulala.
Aliwataka
majeruhi kuwa ni Rashid Juma (18), Omari Juma (15) na Hamad Juma (11) ambao
wote wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa matibabu.
Alisema
uchunguzi wa awali wa tukio hilo ni kibatari ambacho kiliripuka na kuwasha nguo
ambazo zilikuwa karibu na kusambaa mpaka kwenye vitanda na kuunguza magodoro ya
usufi.
“Mtoto wa
miaka sita na mzee wa miaka hamsini wamekufa baada ya nyumba waliyokuwemo ndani
kuungua yote kwa kushindwa kujinasua na moto ambao ulikuwa ukisambaa kwa kasi”
alisema Wakulyamba na kuongeza
“Wakati
wenzao wakijinasua kutoka katika nyumba ambavyo walikuwa wamelala wao chumba
chao kilikuwa moto umeshauzingira kwani walikuwa chumba kimoja na chanzo ni
kibatari ambacho kiliripuka na kuunguza nguo ambazo zilikuwa karibu” alisema
Katika
tukuio jengine mkazi wa Chumbageni Tanga, Hamis Hamad (46) amefariki baada ya
watu wasiojulikana kumshambuliwa kwa mawe na marungu kwa tuhuma za wizi.
Alisema
kijana huyo ambaye alituhumiwa kuiba vifaa vya ndani ikiwemo Tv na Radio usiku
wa saa 9 eneo la Chumbageni kwa kutumia baskeli na ndipo walinzi walipopiga
kelele za mwizi.
‘Huyo kijana
ni mwizi mzoefu na kw amuda mrefu polisi walikuwa wakimsaka kwa udi na uvumba
kumsomea mashtaka na kumfikisha mahakamani na usiku wa kuamkia leo taarifa ni
kuwa ameuwawa” alisema kamanda
Kamanda
Wakulyamba amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikoni na badala yake
watuhumiwa kuwafikisha polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Mwisho
No comments:
Post a Comment