Tangakumekuchablog
Tanga, CHAMA Cha Viziwi Tanzania (Chavita)
Kimeikumbusha Serikali kuwawekea wakalimani wa lugha za alama katika
Televisheni ili kuweza kupata habari za Bunge na za kitaifa na Kimataifa na
kuacha kusimuliwa.
Akizungumza katika Kongamano la Wajasiriamali Viziwi
kuhusiana na kujiunga na Mifuko ya Bima, Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa ,
Nibros Mlawa, amesema walemavu wa kusikia wamekuwa wahanga wa kukosa habari
kwa muda mrefu.
Ameliomba Bunge kupitisha sheria ya kila Televisheni kuweka
mkalimani wa lugha za alama jambo ambalo litasaidia kupata na kujua matukio
yanayojiri na kuepukana na kupata habari za kusimuliwa ambazo nyengine hazina
ukweli.
Akikumbushia walemavu kujiunga na mifuko ya jamii, Mlawa
amesema walemavu wako tayari kujiunga na mifuko hiyo lakini kwanza kuboresha
miundombinu ya kuyafikia matibabu ikiwemo kuweka ngazi maalumu kwa walemavu na
barabara.
Afisa Jinsia na Maendeleo Makao Makuu ya Chama Cha Viziwi Tanzania (Chavita), Lupi Mwaisaka, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa warsha ya Wajasiriamali Viziwi kupata elimu ya kujiunga na Bima ya Afya , kulia ni mkalimani wa kituo cha watoto walemavu (YDPC), Prisca Mwakasendile.
Kwa habari , matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment