HADITHI Inaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Kampuni ya Usafirishaji abiria ya Freys Coach ifanyayo safari Tanga, Moshi, Arusha, Babati hadi Singida moja kwa moja kila siku, Ofisi za Freys zipo Tanga barabara ya 12, simu 0622 292990
YAMENIKUTA SALAMA MIE 2
ILIPOISHIA
Wakati nimekaa nje ya chumba
cha daktari nikiwaza, daktari alitoka na kuuliza.
“Aliyemleta huyu majeruhi
aliyegongwa na gari ni nani?”
Hapo hapo nilishituka
nikajua kuwa msichana ameshakufa.
Nilikuwa nimekaa na watu
wengine wanne waliokuwa na shida zao. Nikainuka na kumjibu yule daktari.
“Ni mimi”
“Majeruhi amepoteza damu
nyingi na anahitaji kuwekewa damu ili kuokoa maisha yake. Na hapa tumeishiwa na
damu” akaniambia.
“Sasa tutafanyaje daktari?”
“La kufanya ni kupatikana
damu kutoka kwa mtu yeyote, kwani ndugu zake wako wapi?”
“Siwatambui. Kama yangu itafaa niko tayari kumsaidia”
“Haya twende tukakupime kama unaweza kumtolea”
SASA ENDELEA
Daktari huyo alinipeleka
katika chumba cha maabara. Nilitolewa damu yangu kwa ajili ya kuchukuliwa
kipimo.
Niliambiwa kwanza
ingechunguzwa ili kuonekana kama ilikuwa salama na kama
nina damu ya kutosha kumpatia mtu mwingine.
Nilisubirishwa kwa karibu saa
nzima kabla ya kuambiwa kuwa damu yangu ilikuwa salama na nilikuwa na uwezo wa
kumtolea yule msichana.
Nilifurahi sana nilipoambiwa hivyo kwani muda wote
nilikuwa nikimsikitikia msichana huyo.
Kikubwa kilichokuwa
kikinisikitisha ni kwamba sikutaka afe. Baada ya damu yangu kutolewa nilipewa
kikombe cha chai ya maziwa ili kiniweke sawa.
Wakati nakunywa chai, damu
niliyotoa ilipelekwa katika chumba alichokuwa
yule msichana. Baadaye kidogo polisi wa usalama barabarani wakafika.
Nilikuwa nimeshamaliza kunywa
chai na polisi hao walikuwa wameshapewa maelezo na wafanyakazi wa hospitali.
Wakanitaka na mimi niwape
maelezo, nikawaeleza jinsi ajali ilivyotokea na jinsi nilivyomchukua huyo
msichana na kumleta hapo hospitali.
“Tumeambiwa kuwa alikuwa
anahitaji kuwekewa damu na uliamua kumsaidia?” Polisi mmoja akaniuliza.
“Ndiyo nimemtolea damu”
“Sijui kama unamfahamu huyu
msichana?”
Nikatikisa kichwa.
“Kwa kweli simfahamu”
“Je ile gari iliyomgonga
uliiona?”
“Ndiyo niliiona”
“Unaweza kututajia aina yake
na namba yake ya usajili”
“Ni Toyota ya rangi nyeupe.
Namba yake ya usajili sikuiona yote. Niliona namba za mwanzo tu”
“Tutajie hizo hizo”
Nikawatajia.
“Umetusaidia. Kuna mtu aliona
namba zinazofuatia. Mtu mwingine alikariri tarakiu zote. Sasa tutakuwa tumepata
namba kamili. Ninaamini tutalikamata hili gari muda usio mrefu”
“Mkimpata huyo dereva ni
vyema anyang’anywe leseni kabisa. Ni dereva katili sana”
“Tukimpata tutamfikisha
mahakamani. Mahakama ndio yenye uamuzi”
“Sawa”’
Baada ya kuzungumza na polisi
hao daktari alinifuata na kuniambia kuwa ninaweza kuondoka kwani majeruhi niliyempeleka
anaendelea kuwekewa damu.
“Ameshazinduka?” nikamuuliza.
“Hajazinduka bado lakini
tunatarajia kuwa atazinduka muda si mrefu. Tunaendelea kumfanyia uchunguzi
kuona kama ameumia kwa ndani”
“Sawa. Nitakuja kumuangalia
kesho asubbuhi”
“Vizuri”
Wakati natoka hapo hospitali
jua lilikuwa limeshakuchwa. Nilimpigia simu Zacharia nikamuuliza.
“Uko wapi?”
“Niko ofisini?”
“Hamjafunga ofisi bado?”
“Ndio tunataka kufunga”
“Basi fungeni, mimi sitafika
tena huko. Tutakutana nyumbani”
“Sawa kaka”
Nikajipakia kwenye gari na
kurudi nyumbani.
Asubuhi ya siku ya pili yake
nilipotoka nyumbani nilikwenda hospitali ya Bombo kumjulia hali yule msichana.
Nilifurahi kumkuta
akizungumza na muuguzi aliyekuwa akimhudumia.
“Oh kaka umefika tena?” yule
muuguzi aliniuliza akikumbuka kwamba ndiye mimi niliyemleta hospitali yule
msichana jana yake.
“Ehe nimefika kumjulia hali
mgonjwa wangu” nikamjibu huku nikitabasamu.
“Mgonjwa wako anaendelea
vizuri, Jana tumemuwekea damu na jana hiyo hiyo alizinduka”
Wakati nikizungumza na yule
muuguzi yule msichana alikuwa akinitazama kwa macho ya shauku na udadisi.
“Salma huyu ndiye yule kaka
aliyekuleta hospitali” Muuguzi huyo akamwambia.
Msichana huyo akashituka.
“Ndiye huyu kaka? Nimefurahi
kumuona”
Msichana akanitazama kwa
macho ya bashasha na kuniammbia.
“Asante
kaka, nnakushukuru sana
kwa msaada wako. Mungu atakulipa”
“Ni watu wachache sana duniani wenye moyo kama
wake, kuacha shughuli yake na kukushughulikia wewe mtu ambaye hakufahamu na
zaidi ya hapo akutolee damu iliyoweza kukusaidia hadi leo unajisikia vyema”
Yule muuguzi akamwambia.
“Ni moyo wa kibinaadamu kweli
kweli. Kwa kweli namshukuru sana.
Mimi sina cha kumlipa ila Mungu ndiye atakayemlipa”
“Asante mdogo wangu kwa shukurani
zako. Nimekuja kukujulia hali nijue unaendeleaje kwa sababu jana niliondoka
ukiwa bado hujitambui”
“Kwa kweli kaka naendelea
vizuri, nashukuru Mungu”
“Mimi naitwa Ibrahim Amour,
ni mkazi wa Usagara hapa Tanga, sijui
wewe mwenzangu unaitwa nani?”
“Naitwa Salma Aboud”
“Unaishi wapi?”
“Ninaishi Chumbageni”
“Unaishi na wazazi?”
“Ninaishi na mama yangu, Baba
yangu alishafariki”
“Kwa hiyo mama ayko anayo
taarifa kuwa umepata ajali?’
“Mama hayuko, amekwenda
kijijini tangu juzi”
“Basi atakuwa hana habari”
“Atakuwa hajui”
“Alikwambia angerudi lini?”
“Atakuwa huko kwa wiki nzima”
“Si kitu, nitakuachia namba
yangu ya simu, ukiwa na tatizo unaweza kunipigia”
ITAENDELEA kesho usikose uhondo huu hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment