Friday, September 16, 2016

NJIA ZA KUMTABUA MTU ALIEFARIKI

HIZI NDIO NJIA NANE ZA KUMKAGUA MGONJWA WAKO AU MTU YEYOTE KAMA AMEFARIKI KWELI

kumekua na ripoti nyingi na matukio ambayo inatokea mtu anazikwa kabla hajafa, hasa sehemu za vijijini sana ambapo hakuna madaktari au wahudumu wa afya. kwa sheria za tanzania, mgonjwa akifia hospitali basi dakatari ndio anaruhusiwa kukagua na kuhakikisha kweli mgonjwa huyu amefariki kabla ya kwenda kuzikwa. elimu hii ya kujua kama mgonjwa bado yuko hai au amekufa ni vizuri ikatolewa kwa watu wote ili kuepusha matukio hayo ya kuzika watu walio poteza fahamu tu wakidhani ni wafu.zifuatazo ni dalili hizo...

kusima kwa mfumo wa upumuaji;muangalie mtu kifuani kisha kua makini, kwa mtu aliyepoteza fahamu utaona kifua kinapanda na kushuka lakini kwa mtu mfu utaona kifua kimetulia kabisa na hakuna dalili za kupumua hata kwa mbali.

kusimama kwa mapigo ya moyo; haya unaweza kuyasikia kwa kutumia kifaa maaluma kwa jina la stethoscope lakini kwa mtu wa kawaida ambaye sio mtaalamu basi weka sikio lako upande wa kushoto mwa kifua cha mtu  na kama husikiii mapigo ya moyo huyu mtu ni mfu.

msukumo wa damu; hii kitaalamu inaitwa pulse rate,kwa kutumia vidole vyako viwili vya mkono wako kandamiza kidogo sehemu ya mkono ambapo kuna kidole gumba. kwa kawaida utahisi damu inapita na inasukuma vidole vyako na kama husikii kabisa basi huyo ni mfu.pia unaweza kuweka vidole shingoni kama wafanyavyo askari mara nyingi kukagua kifo.



 angalia jicho; jicho lina duara mbili nyeusi, moja ni kubwa na nyingine ndogo kabisa kitaalamu tunaita pupil. kwa hali ya kawaida pupil ukipiga tochi ghafla nasinyaa na ukitoa tochi inapanuka kawaida. sasa kwa mfu hautaona hayo mabadiliko lakini pia pupil yake itakua imepanuka kuliko kawaida.angalia tofauti kwenye picha hizi mbili.
kukakamaa sana; kutokana na kusimama kwa kazi ya mishipa ya fahamu, mfu hukakamaa sana muda tu baada ya kufa na usipowahi kumnyosha basi anaweza asirudi kwenye hali ya kawaida.

kuwa wa baridi; inategemea na muda wa kifo lakini mara nyingi masaa nane baada ya kifo mtu huanza kuwa wa baridi sana kuliko kawaida hasa miguuni kutokana na kupotea kwa joto la kawaida la kiumbe hai.

kuanza kutoa harufu kali; vitu laini sana kwenye mwili wa binadamu kama ubongo na utumbo huanza kuoza haraka mtu anapokufa, hivyo harufu kuotekea sehemu zote zenye mashimo kama pua, mdomo, na sehemu za siri huanza kutoka.

kutosikia maumivu kabisa; mfinye sana mgonjwa miguuni au mkononi au sehemu yeyote yenye nyama lakini hautaona ushirikiano wowote.

mwisho; kuna njia zingine za kujua kifo ambazo zinatumia vifaa maalumu na zingine huwezi kuzielewa kama wewe sio daktari, lakini ukiona dalili zote hizo kwa mgonjwa kwa uhakika basi unaweza kusema amefariki japokua ni vizuri kumuita na daktari ahakikishe ila kama ni kijijini sana basi mnaweza kuzika.unaweza kubonyeza maneno ya kijani kwa maelezo zaidi na kupitia blog yangu ya kingereza.

mgblog

No comments:

Post a Comment