Idadi ya wahamiaji waliozama kutoka Misri yaongezeka
Lilikuwa linawasafirisha raia wa Misri, Syria, Sudan, Eritrea na hata wahamiaji wa Somalia.
Maafisa wanasema kiasi ya watu 163 wameokolewa lakini walionusurika wameiambia BBC kuwa mamia wengine huenda wamezama.
Washukiwa wanne wamekamatwa na polisi kwa kushukiwa kwa mauaji yasio ya makusudi na usafirishaji haramu wa binaadamu, maafisa wa Misri wanasema.
Boti hilo lililo ondolewa kutoka pwani kwa siku tano wakati wahamiaji zaidi walipoletwa, linasemekana kuzama baada ya kundi la mwisho la watu 150 kujazwa ndani.
Mkasa huo unatokea wakati shirika la kulinda mpaka wa Umoja wa Ulaya limeonya kuwa idadi inayoongezeka ya wahamiaji wanaoelekea Ulaya wanatumia Misri kama eneo la kuondoka.
Zaidi ya watu 10,000 wamefariki wakivuka bahari ya Mediterrania kuelekea Ulaya tangu 2014, kwa mujibu wa Umoja wa mataifa.
No comments:
Post a Comment