Darubini kubwa kuliko zote duniani yaanza uchunguzi wa Sayari na Nyota
Darubini kubwa kuliko zote duniani itakua inafananaje? Leo
nakusogezea taarifa hii kutoka China juu ya Darubini kubwa zaidi duniani
ambayo leo Sepetember 25, 2016 imeanza uchunguzi wa sayari na nyota
katika mkoa wa Guizhou ulioko kusini magharibi mwa China.
Leo
mchana, mamia ya wanaanga na mashabiki wa mambo ya anga wameshuhudia
kuanza rasmi jukumu la darubini hiyo la kuchunguza anga la juu na
kutafuta kama kuna maisha katika anga hiyo.
Mradi wa
ujenzi wa darubini hiyo umeigharimu China kiasi cha dola za kimarekani
milioni 180 na ulianza mwaka 2011, ikiwa ni miaka 17 baada ya
kupendekezwa na wanaanga wa China.
Rais Xi
Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa wanasayansi, wahandisi, na
wajenzi wa darubini hiyo mara ilipoanza rasmi kufanya kazi hii leo.
millrdayo
No comments:
Post a Comment