Tangakumekuchablog
Muheza, BAADHI
ya familia kijiji cha Kirapula kata ya Ngomeni Muheza Tanga wamelazimika
kuyahama makazi yao kufuatia kero ya maji ilichokikumba kijiji chao kwa muda
mrefu.
Pia familia hizo wamesema ndoa zao
huingia katika migogoro kwa kulazimika kuamka saa tisa usiku ili kuwahi foleni
ya maji kwenye kisima kimoja ambacho maji yake hayana uhakika .
Wakizungumza na waandishi wa habari
kijijini hapo leo, familia hizo wamesema wamelazimika kuzihama nyumba zao kuepuka
kuzuka kwa magonjwa ya miripuko ukiwemo wa matumbo na kichocho.
“Kero yetu hapa ni ya muda mrefu na
viongozi wetu wanajua na tumekuwa tukipewa ahadi kila siku, kwa sasa subira
imezidi na ni bora kujisalimisha kuepuka magonjwa” alisema Sofia Hassan na
kuongeza
“Watoto wetu wamekuwa wakienda shule
bila kuoga na nguo chafu jambo ambalo linawalazimu baada ya kutokuwa na njia
mbadala ya kupata maji na hilo linarudisha nyumba uelewa wa masomo darasani”
alisema
Kwa upande wake Diana Hassan,
alisema kero hiyo ya maji imekuwa ikiwaingiza katika migogoro ya ndoa na waume
zao baada ya kulazimika kuamka saa tisa usiku kuwahi foleni katika kisima
kimoja kilichopo pekee.
Alisema baadhi ya siku husindikizwa
na waume zao na siku nyengine waume hugoma kuamka jambo ambalo hupelekea kutoka
peke yao hivyo unapochelewa kurejea hupatwa na maswali.
“Kero ya maji inatuingiza katika
mizozo na waume zetu kwani unapochelewa unapatwa na maswali mengi huku
ikieleweka wazi kuwa hukumbana na foleni
hata uamke saa nane usiku” a;lisema Diana
Nae Bakari Mauya, alisema hulazimika
kuamka usiku wa saa kumi pamoja na familia yake na watoto na kila mmoja hubeba
ndoo moja ambayo hutumia hadi siku ya pili.
Alisema hupata nafuu vipindi vya
mvua kwa kuhifadhi katika mapipa na ndoo na kuepukana na adha ya utafutaji maji
usiku na kusema kuwa endapo ukichelewa unaweza kukosa maji ya kutumia mchana
mzima.
Alisema ili kuweza kuzinusuru afya
na wakazi wa Kilapula na kubaki katika makazi yao Serikali kuweza kuwawekea
kisima cha maji safi ambacho watakuwa na uhakika wa upataikanaji na kuepukana
na adha ya kuamka usiku wa manane.
Mwisho
No comments:
Post a Comment