Tanga.Serikali inatarajia kuzindua
mpango maalumu wa kupambana na uchafuzi wa bahari ikiwa ni njia ya kukabiliana na changamoto
itakayotokana na ongezeko la meli kubwa zitakazokuwa zikitia nanga katika
bandari za Tanzania bara na Zanzibar.
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wan chi kavu na majini (Simatra),Captain Mussa
Mandia alisema hayo leo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari
kuzungumzia maadhimisho ya wiki ya
bahari duniani yanayofanyika kitaifa jijini Tanga.
Alisema Serikali ya Jamahuri ya
Muungano wa Tanzania imeandaa mpango maalumu wa kupambana na uchafuzi wa bahari
(NMOSCRP) ambao utaviwezsha vyombo vinavyohusika na bahari kuhakikisha
mazingira ya bahari hayachafuliwi.
“Serikali ya awamu ya tano imeazimia
kuendesha uvuvi wa kisasa katika bahari ya hindi na maziwa yake kwa maana hiyo
ni wazi kwamba zitakuja meli kubwa kuvua,kama hatutaweka mpango wa kudhibiti
uchafuzi bahari yetu itachafuliwa sana”alisema
Mandia.
Alisema uzinduzi wa mpango huo
utafanyika wiki hii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya bahari dunia
ambapo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzui na mawasilianoProfesa Makame Mbarawa atakuwa
mgeni rasmi.
Selemani Musa Makame kutoka Mamlaka
ya meli Zanzibar (ZMA),alisema katika uzinduzi huo,Waziri wa Biashara ,Amina
Salum Ali ataiwakilisha Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar katika uzinduzi huo.
MWISHO
,Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) Mussa Mandia, akizungumza na waandishi wa habari Tanga jana kuzungumzia mpango wa maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Devid Mzirai, Meneja Mawasiliano Sumatra.
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wan chi kavu na Majini (Sumatra) Mussa Mandia, akizungumza na waandishi wa habari jana kuzungumzia mpango maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kulia ni Mkurigenzi Mkuu Mamlaka ua Usafiri Baharini Zanzibar, Suleiman Massoud.
Waandishi wa habari wakichukua habari wakati w amkiutano wa waandishi wa habari leo
Mwandishi wa habari wa Radia Huruma ya Tanga, Pamela Chaullah akiwajibika wakati wa mkutano leo
No comments:
Post a Comment