Morocco imewasilisha rasmi ombi la kutaka kujiunga upya na AU
Muungano wa Afrika unasema Morocco imewasilisha rasmi ombi la kutaka kujiunga tena na muungano huo.
Morocco
ilijitoa katika lililokuwa Shirika la Muungano wa Afrika OAU, zaidi ya
miongo mitatu iliyopita kufuatia mzozo kuhusu eneo la Magharibi mwa
Sahara Muungano wa Afrika umelitambua eneo hilo kama taifa huru, wakati Morocco inalitazama kama sehemu ya eneo lake.
Muandishi wa BBC anasema inaonekana kuwa Morocco sasa inatambua kutokuwepo kwake kumepunguza ushawishi wake Afrika.
Inatarajia kuwa kwa kujiunga kwa mara nyengine na muungano wa Afrika itasaidia kuipa nafasi zaidi ya kushawishi mataifa mengine kuunga mkono msimamo wake kuhusu sehemu ya Magharibi mwa sahara
BBC
No comments:
Post a Comment