Muheza, VYUMBA vitatu vya madarasa shule ya
msingi Kilulu Wilayani Muheza Mkoani Tanga vimefungwa kufuatia uchakavu wa
majengo yake na mabati kutoboka na kuwa
kero wakati wa mvua na jua.
Shule hiyo
ambayo imejengwa toka mwaka 1950 kwa nguvu za wananchi pia choo kimebomoka hali
inayohatarisha afya za wananchi na usalama wao baada ya shimo hilo refu kutoa
harufu kali.
Akizungumza
na waandishi wa habari , Afisa
mtendaji kata ya Kilulu, Jonathan Siafu, alisema kufuatia hali hiyo wanaiomba
Serikali na wadau wa elimu kuisaidia ili kuwawezesha watoto kusoma kwa utulivu
na kuepuka kujazana darasa moja.
Alisema hali
ya uchakavu wa majengo umekuwa wa muda mrefu na wananfunzi kuwa katika wakati
mgumu hasa wa mvua ambapo hunyeshewa hali ambayo inalazimika kuwahamisha vyumba
vyengine na ufundishaji wake huwa wa
mashaka.
Kwa upande
wake Diwani wa kata hiyo, Hashim Kiango (CCM), alisema kwa sasa shule imefikia
hali mbaya ambapo baadhi ya wakati wanafunzi hudondokewa na vipande vya mabati
na miti ambayo imeliwa na wadudu.
Alisema
inawalazimu kuitisha mkutano wa wananchi ambapo watafanya harambee lengo likiwa
ni kuinusuru ili isianguke na kuwa kero kwa wanafunzi kwa kukosa masomo na kupatiwa uhamisho kusoma
shule nyengine.
“Shule hii
iko barabarani ni mbele ya macho kwa kila apitae hapa na sijui kwa nini kwa muda mrefu hakuna hatua yoyote ya
kuinusuru, hii ni aibu kwetu kwani bado elimu hatuipi kipaumbele” alisema
Kiango na kuongeza
“Kila mgeni
anaepita hapa huishangaa na kupiga picha kama kwamba shule imefungwa au inasubiriwa
kukarabatiwa, na kila siku hali inazidikuwa mbaya na hakuna hatua yoyote ya
kuinusuru” alisema
Kwa upande
wake mwenyekiti wa kijiji cha Enzi, Haruni Mussa, alisema shule hiyo
imesahauliwa hadi kufikia milango na madirisha kudondoka jambo ambalo ni aibu
kwa mustakabali wa elimu.
Alisema
milango na madirisha yameng’oka hivyo kutokuwa na udhibiti wa wanafunzi na
usalama wakati wa usiku kwa vifaa vya shule na vyawanafunzi hivyo kutaka wadau
wa elimu kuiangalia kwa jicho la pili.
“Shule haina
milango wala madirisha na nyakazi zausiku kutokuwa na usalama wa vifaa vya
shule na vya wanafunzi na kuwa hatari” alisema Mussa
Ameitaka
jamii kuiangalia shule hiyo kwa jicho la pili na kuinusuru elimu kwa watoto wao
na kwa taifa kwa jumla kuwa msaada kwa maisha ya vijana wao baadae.
Mwisho
Diwani kata ya Kilulu Wilayani Muheza Mkoani Tanga, Hashim Kiango pamoja na viongozi wengine wa kijiji wakiangalia moja ya vyumba vya madarasa matatu yaliyochakaa na kulazimika wanafunzi kuhamishwa kwa usalama wao.
Diwani wa kata ya Kilulu Wilayani Muheza Mkoani Tanga, Hashim Kiango na mwenyekiti wa kitongoni cha Kilulu, Omary Jumanne, wakiangalia shimo la choo cha shule ya msingi ya Kilulu kilichobomoka na kuwa hatari kwa usalama na afya za wananfunzi shuleni hapo.
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment