Wakazi wa kijiji cha Pingoni kata
ya Pongwe Tanga wakipita kwa shida daraja la Chote ambalo kingo na mbao
zimeibwa na watu wasiojulikana na
kuhatarisha usalama wa watumiaji wa daraja hilo ambalo ndio njia pekee ya
kuelekea ng’ambo ya pili. Daraja hilo ambalo lilijengwa na wakoloni linatumika
hadi leo hii.
Daraja hilo lililojengwa na Wakoloni mwaka 1950 hadi leo limekuwa likitumika ila kuna baadhi ya watu ambao sio waaminifu wamekuwa wakikata vyuma na kuviuza kama chuma chakavu.
Hali hii imekuwa hatarishi hasa vipindi vya mvua kubwa ambao chini kuna mamba na kuhatarisha usalama wa wananfunzi waendapo shule na wapita njia pamoja na kuwa daraja hilo ndilo pekee la kupitia na kusafitrisha mazao pamoja na wafanyabiashara wa mkaa.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment