Friday, September 23, 2016

UWAMTA TANGA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWASAIDIA



Tangakumekuchablog

Tanga, UMOJA wa Wajasiriamali mjini Tanga (Uwamta) umemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati sakata la kitisho cha kutaka  kuhamishwa kwa nguvu na watu walilodai kuwa ni kutoka Fax Auction Marts katika jengo la karakana ambapo wapo watu zaidi ya 200 wanaoendesha kazi zao na kutoa ajira kwa vijana.
Jengo hilo lenye karakana mbalimbali zikiwemo za uchomeleaji, ufundi wa magari na uchongaji vyuma wamedaiai kuwepo kwa zaidi ya miaka 25 jengoni hapo  walilopewa na Serikali wakati wa ubinfsishaji kwa kupewa vyama vya ushirika.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana, Umoja huo umesema endapo Serikali italifumbia macho sakata hilo kuna dalili za kuwpo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani jambo ambalo halitakikani kutokea.
“Tumekuwa tukipewa vipeperushi na vitisho vya kutakiwa kuondoka katika eneo letu ambalo liko na karakana pamoja na mashine za kusagia vyuma pamoja na ufundi wa magari kwa zaidi ya miaka ishirini na tano” alisema Tyson Elyakim ambaye ni mwenyekiti wa umoja huo na kuongeza
“Hapa tupo zaidi ya watu mia mbili ambao tunaendesha kazi mbalimbali na kutoa ajira kwa vijana ambao baada ya muda hujiajiri wao wenyewe baada ya kupata ujuzi na sasa kujitokeza mtu mmoja kututaka kuondoka bila kuwa na vigezo hujko ni kutunyanyasa” alisema
Alisema karakata hiyo imetoa vijana wengi ambao kwa sasa nao wanatoa ajira kwa vijana wenzao ambao hawana kazi na kusema kuwa kuwepo kwao kumesaidia vijana kuacha kujitumbukiza katika mambo ambayo hayana maana.
Kwa upande wake, Mjasiriamali mama lishe, Rehema Juma ambaye hufanya biashara zake kwa kuwauzia wafanyakazi alisema kuna kikundi ambacho humwaga vipeperushi nyakati za usiku jambo ambalo limekuwa likiwarusisha nyuma nguvu kazi.
Alisema wamekuwa wakifanya shughuli zao kwa woga ambapo badhi ya wakati wamekuwa wakipokea vipeperushi vya kutakiwa kuondoka chini ya siku saba ambapo mtoaji wa taarifa haonekani.
Alisema hali hiyo imekuwa ikirudisha nyuma nguvu kazi na  hivyo kumuomba Rais kuingilia kati unyanyasaji ili vikundi hivyo vya wajasiriamali wanawake waweze kujikwamua na umasikini badala ya kuwategemea waume zao.
                                                 Mwisho






Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment