Cheki na majibu ya utafiti wa uaminifu wa watu wa Dubai… Naambiwa na Afrika itafika hii!
Jamaa mmoja ambaye ni mtengeneza Filamu raia wa Uingereza amefanya utafiti katika mitaa ya Dubai, utafiti ulioitwa “Je unaweza kuiba Dubai?” kwa lengo kuangalia jinsi gani watu wa maeneo ya huko ni waaminifu.
Jamaa huyo Daniel Jarvis, akiwa na rafiki yake walianza utafiti huo hivi karibuni kwa kuficha camera na kurekodi mfululizo wa matukio, Daniel anapita mtaani halafu anaangusha wallet yake makusudi kabisa, ili kuangalia wale watakaoiona watachukua uamuzi gani?
Mtaa wa kwanza walioufanyia majaribio hilo ni katika barabara ya Sheikh Zayed karibu na Soko Kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara wa Emirates, kila aliyeiona wallet hiyo
alimrudishia, akahisi huenda sababu ya kurudishiwa pochi hiyo ni
kutokana na wakazi wa eneo hilo kuwa matajiri, wakaamua kuhamishia
utafiti huo eneo la Bur, ambalo watu wa maeneo hao ni wale wenye kipato cha kawaida, cha kushangaza watu hao pia walimrudishia.
Kikubwa kilichomshangaza katika utafiti
huo ni kwamba hata watu waliookota pochi hiyo hawakujishughulisha
kutazama ndani kuna nini, walimuita na kumpatia!
Kampuni hiyo ya utafiti ya Trollstation
inaendelea na utafiti wake katika Falme za Kiarabu, Ulaya, Marekani na
hatimaye Afrika ambapo wamesema huenda maeneo watakayopita yakavunja
rekodi ya Dubai.
Nasubiri kama utafiti huu ukifika Tz, maeneo ya watu wengi kama Kariakoo, Stendu pale Arusha na Mwanza na pia Tanga eneo la Ngamiani na Tangamano unadhani hali itakuwaje mtu wangu?
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment