Mengine kutoka Kenya kuhusu ishu ya ndoa za jinsia moja… Story iko hapa kwenye audio
Ni mjadala ulioanza mwaka 2010 Kenya
ilipojipatia Katiba mpya, mjadala uliotokana na ishu ya mwaka 2010
haionyeshi wala kutoa mwelekeo bayana kuhusu hatima ya watu
wanaojihusisha na uhusiano wa jinsia moja.
Chama cha siasa cha Republican Liberty Party (RLP) kinatishia kumchukulia hatua Spika wa Bunge Kenya, Jastin Muturi
ikiwa muswada wa Sheria ya kupinga uhusiano wa jinsia moja 2014
hautaanza kujadiliwa wakati ambao Bunge hilo litakapoanza vikao vyake
mwezi ujao.
Ripota wa tangakumekuchablog kutoka Kenya,amezungumza na kiongozi wa chama hicho, Vincent Kidaha kuhusu
vipengele vilivyomo kwenye sheria hiyo ambavyo vinaeleza hukumu ya mtu
yeyote atakayetetea au kujihusisha kwenye uhusiano ya jinsia moja.
Akizungumzia ishu hiyo Kidaha amesema; “Baadhi
ya vipengele ambavyo tunawasilisha ni kwamba kwa wale washoga ambao
wanaleta tabia za ushoga Kenya kama ni kutoka nchi za kigeni waweze
kupewa adhabu ya kupigwa mawe na kama ni wakenya wahukumiwe kunyongwa
sasa hiyo ni baadhi ya vipengele ambayo tunataka kurekebisha taifa letu
liweze kurudia maadili ya kijamii“– Vincent Kidaha.
No comments:
Post a Comment